Na Hamisi Miraji,TimesMajira Online
Benki ya Uwekezaji Ulaya (EIB), inatarajia kukuza Uwekezaji wa Shilingi trilioni 1.8 nchini Tanzania kwa ajili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mwaka huu, zaidi ya TZS bilioni 454 (euro milioni 170) za uwekezaji wa EIB zimetolewa kwa SMEs kwa kuzingatia miradi inayoongozwa na/inayomilikiwa na wanawake.
Mbali na hivyo benki hiyo, pia ilitia saini ufadhili mkubwa zaidi kwa uchumi wa bluu duniani, ikitoa zaidi ya TZS bilioni 267 (euro milioni 100) kwa nchi.
Wawakilishi kutoka Benki ya Uwekezaji Ulaya (EIB), kanda ya Afrika Mashariki hivi karibuni walihitimisha ziara yao kwa kutembelea Wizara ya Fedha na Mipango Tanzania kwa ajili ya kujadili njia za kuongeza uwekezaji nchini.
Akizungumza mara baada ya wawakilishi hao kutembelea Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania, Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Fedha za Umma hapa nchini, Amina K. Shaaban amesema Tanzania inaikaribisha EIB kwa mijadala yenye manufaa kwa nchi.
“Tunakaribisha EIB kwa mijadala yenye manufaa ambayo tumekuwa nayo kuhusu miradi ya maendeleo na tunaweza kushirikiana nao. Ziara yao kwa sasa inafanyika kwa wakati mwafaka kwani kwa sasa Tanzania, inasasisha Dira yake ya Maendeleo ya 2050 kutoka ya sasa ambayo itakamilika 2025,” amesema Amina.
Amina ameisifu kazi ambayo EIB Global inafanya kuhusu kutoa usaidizi wa uwekezaji kwa miradi inayoongozwa na wanawake au inayomilikiwa na wanawake, kwa msaada wa EU.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa EIB, Thomas Ostros amefurahishwa sana na timu ya EIB, kutoka kituo kikuu cha kanda ya Nairobi inayofuatilia miradi huku wakiunga mkono serikali katika kuitekeleza.
“Nimefurahishwa sana na timu ya EIB kutoka kituo kikuu cha kanda ya Nairobi, inafuatilia miradi ambayo tungependa kuunga mkono serikali katika kuitekeleza.
“Mfumo wetu wa biashara unaangalia kuhakikisha kuwa tunashirikiana na serikali katika kufikia malengo ya maendeleo ya pamoja ambayo pia ni vipaumbele vya serikali vinavyoboresha maisha ya wananchi,” amesema Ostros.
EIB Global ni taasisi ya muda mrefu ya Umoja wa Ulaya inayomilikiwa na Nchi Wanachama na ndiyo taasisi kubwa zaidi ya kimataifa duniani.
Taasisi hiyo inafadhili uwekezaji kote ulimwenguni ikiwa ni pamoja na Afrika katika maeneo ya kipaumbele ikiwemo miundombinu, uwekaji wa digitali na uvumbuzi, hatua za hali ya hewa na nishati pamoja na maendeleo ya biashara ndogo na za kati.
Baada ya kuwekeza katika miradi zaidi ya 28 hadi sasa, EIB tayari imetia saini zaidi ya TZS trilioni 1.8 (euro milioni 680) za msaada kwa mipango ya Serikali kwenye sekta ya umma, pamoja na kutoa njia za mikopo kwa benki za biashara na taasisi ndogo za fedha nchini.
Pi, kukopesha makampuni binafsi, hasa SMEs, pamoja na watu binafsi katika sekta binafsi. Kati ya fedha hizo, zaidi ya TZS trilioni 1.34 (euro milioni 500) tayari zimetolewa huku zaidi zikitarajiwa kutolewa wakati miradi inaanza.
Baadhi ya miradi ambayo EIB imesaidia ni Mpango wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Ziwa Victoria mkoani Mwanza, Mradi wa Umeme wa Tanesco, uboreshaji wa Bandari ya Dar-es-Salaam, mtambo wa kufua umeme wa Kihansi na mikopo kwa mabenki ili kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati. hasa, Uchumi wa Bluu na miradi inayoongozwa na wanawake na/au inayomilikiwa.
Hata hivyo, benki hiyo kwa sasa inaandaa miradi mipya ukiwemo mradi wa usimamizi wa taka ngumu jijini Tanga ambao kwa sasa uko katika hatua ya upembuzi yakinifu.
Mradi huo upo chini ya EIB’s Clean Oceans Project Identification and Preparation (COPIP) ambayo inalenga kupunguza kiasi cha taka za plastiki zinazoishia baharini katika miji ya pwani ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Mifano mingine ni uwekezaji wa moja kwa moja katika makampuni ya TEHAMA ili kukuza ujanibishaji wa kidijitali.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba