January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benki ya EQUITY yarahisisha biashara kwa wateja wake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Benki ya EQUITY imeendelea kurahisisha huduma zake katika nyanja zote kwa wadau wote wa biashara nchini kuanzia mtu binafsi, wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa.

Hayo ameyasema Afisa Mwangalizi wa wateja wakubwa Benki ya EQUITY, Adams Marandu wakati akizingumza na waandishi wa Habari katika maonesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba) Jana Jijini Dar es salaam.

“Katika maonesho ya mwaka huu ujumbe wetu mkubwa ni TUMERAHISISHA, tumerahisisha biashara katika nyanja zote kwa wadau wote wa biashara nchini kuanzia mtu binafsi, wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa”

Aidha Marandu amezitaja huduma zote za ndani ya Benki ya EQUITY ambazo zimerahisishwa ikiwemo ufunguaji wa akaunti, utaratibu wa kupata afisa mahususi, upatikanaji wa mikopo na kutoa elimu kuhakikisha kwamba huduma wanayoipata ni sahihi na yenye kutusaidia kukua.

Marandu amewakaribisha wananchi wote katika matawi ya Benki ya EQUITY nchini nzima ili wapate huduma na kupelekea kukuza uchumi wetu wa Tanzania.