Na David John timesmajira online
WIZARA ya Kilimo imepokea kiasi cha Dola 300 sawa na shilingi bilioni 700 za Kitanzania kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo hapa nchini .
Waziri Kilimo Hussein Bashe amebainisha hayo katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo mkutano mkubwa wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Afrika unafanyika.
Amesema,hatua hiyo ni mafanikio kwa nchi kwani Moja ya malengo yake ilikuwa ni kutafuta fedha kwa ajili ya sekta ya kilimo na tayari fedha zimepatikana .
Kwa.mujibu wa Waziri huyo fedha hizo zitaelekezwa zaidi kwenye maeneo ya miundombinu ya umwagiliaji hasa kwa wakulima wadogo.
Pia amesema kuwa kumekuwa na majadiliano ya namna ya kutuza mazingira huku akisema tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kama umasikini wa watu hautaondolewa .
“Kwa hiyo tumezungumza na Benki ya Dunia ambapo tulikuwa na majadiliano nao ya muda mrefu na pia walikutana na mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipokwenda Washington nchini Marekani .” amesema na kuongeza kuwa
“Tumeweza kufikia mwisho na mpango huu unaanza kutekelezwa mwaka huu kwa ajili ya kujenga miundombinu ,ni mpango wa miaka mitano lakini tutajitahidi tutumie fedha hizi ndani ya miaka mitatu na ndicho tulichokubaliana na moja ya makubaliano ni kujenga miundombinu ya umwagiliaji ya zaidi ya hekta 37 hii itasaidia sana kuongeza eneo letu la uzalishaji na bahati nzuri wakati wanakuja wao tayari sisi tulishakuwa na dizaini ya miradi ambayo tunataka kuifanya,
“Kutakuwa na uzinduzi na baada ya hapo tutakuwa tumemalizana na wao na fedha hizi ni mkopo Kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo kwani Kwa muda mrefu mlikuwa mkiona benki ya Dunia inatoa fedha Kwa ajili ya kujenga barabara ,kwahiyo huo ni mradi mkubwa wa kwanza wa fedha ambao tunaupata katika kipindi hiki ambapo hauendi kwenye barabara badala yake unaenda kwenye kilimo Moja Kwa Moja.”amesisitiza Waziri Bashe “
Kwa mujibu wa Waziri huyo,ni Imani yake kwamba fedha hizo zitarekeshwa kutokana na shughuli za kiuchumi na nyingi zipo kwenye sekta yankilimo.
“Tunaamini kwamba hata kama nchi inakopa nchi italipa deni hilo kutokana na shughuli za kiuchumi na nyingi zipo kwenye sekta ya kilimo na ili kuweza kuwafanya wakulima wazalishe vizuri ni lazima kutatua matatizo yanayo waathiri ambayo ni mbegu bora huduma za ugani,miundombinu ya umwagiliaji ili mkulima aweze kuzalisha mara mbili ,mara tatu Kwa mwaka kwahiyo fedha hizo ni mkopo wa muda mrefu lakini unakwenda moja Kwa moja kwenye kilimo.” amesisitiza Bashe
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito