Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Wafanyabiashara wadogo na wakubwa wametakiwa kuchangamkia fursa ya huduma mpya ya ‘Absa Tanzania Mobi Tap’ iliyotolewa na Benki ya Absa ambayo itawasaidia kukuza wigo wa biashara yao na kuwapa nafasi wateja wao kuweza kufanya malipo lakini pia mfanyabiashara kupata maendeleo zaidi.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa kitengo Cha wateja binafsi kutoka Benki ya Absa, Ndabu Swere wakati wakizindua huduma mpya ambayo ni mfumo wa malipo ya Kadi ya kielektroniki ya Benki ya Absa kwa kutumia simu janja inayowawezesha wafanyabiashara wadogo na wakati kuweza kupokea malipo kwa kutumia kadi na simu janja.
“Hii ni njia ambayo tumekuja nayo sisi Absa ambayo ni mpya kabisa Tanzania na inawawezesha wateja hawa kuweza kupokea malipo haya kwa usalama na pia kwa uhakika na wanaweza kuangalia taarifa zao zote za hayo malipo ambayo yameweza kufanyika”
“Sisi kama Absa tunajivunia sana kwa hili hasa kwa vile tumekuwa wa kwanza kuja na huduma hii ambayo ni ya kipekee”
Kadhalika Swere amesema” kumekuwa na njia ya asili ambayo unapokea malipo kwa kutumia kadi na hii njia inahitaji gharama kubwa na uwekezaji na kwasababu inahitajika mashine ambayo yenyewe kuipata ni gharama kubwa ndiyomaana mmekuwa mkiona wateja wakubwa ndiyo wanatumia hii huduma ya malipo lakini kwasababu Absa inasikiliza maoni ya wateja wake tumewaangalia wateja wadogo na wakati ili nao waweze kupokea malipo hayo kwa njia ya kadi.”
Pia amesema Benki ya Absa imejikita katika kuhakikisha kwamba wanaiwezesha Afrika ya kesho kwa pamoja kwa kuwafanya wateja wadogo wanaweza kupata malengo yao, kufanya biashara na kuweza kuzikuzaÂ
“Sisi tunamfikilia mteja wa aina yoyote, mteja mdogo, mkubwa lakini kuna wafanyabiashara wanaofanya biashara ya usafirishaji wanaweza wakatumia huduma hii ambayo anatakiwa awe na simu janja ambapo anaweza kupokea malipo hayo na kuweza kuangalia kwamba amepokea malipo ya kiasi gani na kwa wakati gani” Amesema Swere na kuongeza kuwa
“Wapo wafanyabiashara ambao huwa wanaenda sehemu kwaajili ya kuuza mazao yao, mifugo, biashara ndogondogo n.k lakini watumiaji wanatumia Kadi, hivyo kupitia huduma hiyo mpya itawarahisishia kuweza kupokea malipo hayo kwa usalama na uhakika.”
Kwa upande wa mtumiaji ambaye anaenda kufanya malipo Swere alisema naye pia amerahisishiwa kuweza kufanya malipo kwasababu hatotakiwa kutembea na pesa mkononi ili aweze kufanya malipo hayo.
Swere amewataka wale wote ambao hawajawahi kutumia huduma za Absa waweze kutumia huduma hizo kwani Wana huduma mbalimbali ambazo zinaweza zikamfaa kila mfanyabiashara.
Naye Meneja maendeleo bidhaa za Kadi kutoka Benki ya Absa, Elfrida Mruma amesema Tanzania ni Moja ya nchi inayokua kwa Kasi kuelekea kwenye uchumi wa kati hivyo wao kama ABSA wanaziunga jitihada hizo kwa kuleta njia mbalimbali ambazo zitawasaidia wafanyabiashara mbalimbali ambao ni chachu kubwa ya maendeleo ya uchumi nchini.
Akitaja vigezo ambavyo mfanyabiashara anatakiwa awe navyo, Mruma amesema “Mfumo huu ni njia nafuu sana kwa mfanyabiashara kwasababu vigezo vyake ni vidogo, mteja anatakiwa awe na leseni ya biashara, Tin number na kitambulisho Cha Taifa ambapo kwa vitu hivyo vitatu mteja ataweza kupokea malipo”
More Stories
Simbachawene:Waombaji wa ajira jiungeni na Mfumo wa Ajira Portal
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki