January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bei mpya ya zao la pamba kuwainua kiuchumi wakulima wa zao hilo Shinyanga

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katika mwendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ya kutembelea wananchi katika kata zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga ili kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni pamoja na Kutoa elimu ya Mfumuko wa Bei pamoja na njia ambayo Rais Mama Samia ametumia ya kuweka Fedha za Ruzuku ya Mafuta kiasi Cha shilingi Bilioni 100 ili kuweza kusaidia katika kupunguza Mfumuko wa Bei Nchini .

Juni 14 2022 Mjema akiwa kwenye wilaya ya Kishapu kata ya Mwamalasa Amefanya Mkutano na wananchi wa kata hiyo kwa lengo la Kuwaeleza Namna Ambavyo Serikali imetambua Mchango wa zao la Pamba baada ya Kutoa Bei Elekezi ya Shilingi 1900 hadi 2000 Badala ya Bei ya Awali ilivyokuwa 1560 Ambapo Amesema wananchi wote waliopo katika Kijiji hicho kuhakikisha wanalima kwa wingi zao Hilo la kwani Bei ya Pamba kwa Sasa imekuwa ni nzuri na yenye kumnufaisha Mkulima.

Aidha amesema Rais Mama Samia yupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa dini zote,makabila yote na vyama vyote bila kubagua ndio maana anakuwa na uchungu na wananchi wake
‘ Ndugu zangu wananchi niwaeleze tu ukweli Mama Samia anawapenda mno ndio maana hata Leo mimi mnaniona nimefika hapa ni kwa ajili ya kuja kuwaelezea Yale mengi ambayo serikali yenu imeyafanya lakini muwaepuke wale wanaopita na kuwalaghai kwa maneno kuwa serikali ya awamu ya sita inapandisha Bei za vitu,mara haiwapendi wananchi wake nawaomba muwapuuze hao hawana maana kabisa’ amesema Rc Mjema

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema wilaya yake bado inapongeza jitihada zinazofanywa na Rais Mama Samia katika kuwaletea wananchi Maendeleo hususani kwa kuboresha Upatikanaji wa Elimu pamoja na Huduma ya Afya.

Kwa upande wa wananchi wa Kijiji hicho wamempongeza Rais pamoja na wizara ya Kilimo kwa kuwajali wakulima Wa Mkoa wa Shinyanga na wakulima wote ambao wanalima zao la Pamba kwa kuwa Bei imeboreshwa pamoja na Pembejeo za Kilimo kuletewa kwa wakati, lakini wakatoa Rai kwa serikali kwa kuwaongezea wataalamu zaidi wa Kilimo ili waweze kupewa elimu zaidi juu ya Kilimo Cha Pamba.