December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bechina: Zungu kubadilisha Ilala

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Kalume Hajji Bechina amesema Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu anaibadilisha Ilala kuwa masaki ya kisasa.

Mwenyekiti Hajji Bechina, alisema hayo mtaa wa Kalume Jimbo la Ilala wakati wa kugawa mkono wa Idd kwa wananchi wa mtaa wake ili waweze kufurahi na Familia zao ambapo aligawa Mchele,Sukari, ngano,na tambi kwa kila mwanachi.

“Wananchi wangu wa Mtaa wa Kalume Jimbo letu la Ilala litakuwa la kisasa kwa kufanyiwa mambo makubwa na Mbunge wetu Musa Zungu ambapo Mbunge wetu kwa sasa anajenga barabara za kisasa na miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara ya kisasa ambayo inajengwa na mradi wa DMDP ” alisema Bechina.

Mwenyekiti Bechina alisema Mbunge Zungu anatosha katika nafasi yake ya Ubunge, akichaguliwa Mbunge mwingine Ilala tofauti na Zungu atuwezi kupata maendeleo tena na atuwezi kupata Naibu Spika wa Bunge kutoka Ilala.

Akizungumzia Maendeleo ya Ilala alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesikia kilio cha Ilala Serikali inajenga soko la kisasa Ilala Boma ,Serikali ilipanga kujenga soko la kisasa mwaka 2023 lakini kutokana na changamoto mbalimbali ilishindikana mwaka huu 2024 soko linajengwa .

Wakati huo huo alizungumzia maadili kwa watoto aliwaasa Wazazi wa Ilala kuwalinda watoto wao wakati wote na wasiwaruhusu watoto wao walale na wageni chumba kimoja hata akiwa ndugu yako usimwamini kulala na mwanao usiku.

Kwa upande mwingine ameshauri Serikali ifatilie Ilala wafanyabishara wageni wengi wanatoa viburi na kuizalaru Serikali na hawafuati taratibu kila siku wanavunja sheria.