Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha limefanya operesheni maalum iliyolenga kutoa elimu na kufanya ukaguzi wa mabasi ambayo yatoa huduma Mkoani humo huku likimkamata dereva Sostenes Mgaya 42 Mkazi wa Arusha kwa kosa la kujaza abiria kupita kiasi.
Katika Operesheni operesheni hiyo iliyongozwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Alijua Samutt amesema operesheni hiyo imebaini basi la Kampuni ya Struggle line ambalo amesema limezidisha abiria 33 ambapo alisema kitendo hicho ni kinyume na sheria za Usalama Barabarani huku akibainisha kuwa inahatarisha maisha ya abiria.
ASP Alijua amesema dereva wa basi hilo ameonywa kwa kupigwa faini kwa kosa hilo huku akibainisha kuwa endapo dereva huyo atakamatwa tena kwa kosa hilo ataadhibiwa kwa kufungiwa leseni yake.
Aidha ametoa wito kwa madereva wengine wenye tabia ya kuzidisha abiria kuwa kikosi hicho akitomwonea muhari dereva atakaye bainika kuja abiria kupita kiasi cha uwezo wa gari husika.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba