Na Moses Ng’wat,Timesmajira
WATU wawili wamefariki na wengine 16 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugonga nguzo ya daraja na kutumbukia mtoni.
Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo ambayo imetokea leo Julai 15, 2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Gallus Hyera amesema basi hilo la Ngasere High Class lenye namba T 547 ECX lilikuwa likitokea Dodoma kuelekea katika mji wa mpakani wa Tunduma Mkoani Songwe.
Amesema kuwa basi hilo baada ya kufika eneo la mteremko mkali katika kijiji cha Myovizi, Wilayani Mbozi lilimshinda dereva na kwenda kugonga nguzo ya daraja kisha kutumbukia mtoni na kusababisha vifo hivyo na majeruhi.
Kaimu Kamanda Hyera ameongeza kuwa, katika ajali hiyo watu wawili walifariki papo hapo na wengine 16 walijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ambapo walipatiwa matibabu na kuruhusiwa huku majeruhi wawili wamebaki hospitalini hapo wakiendelea na matibabu kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Kaimu Kamanda Hyera, amewataja waliofariki kuwa ni Henry Msakila (29) na Ipyana Mwaibambe (47) wote wakazi wa Mkoa wa Dodoma.
Aidha, Kaimu Kamanda Hyera amewataja majeruhi wawili ambao bado wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya serikali ya Vwawa iliyopo Wilayani Mbozi kuwa ni Dereva wa basi hilo Salim Mlelwa (42) Mkazi wa Iringa ambaye amevunjika ubavu mmoja pamoja na kondakta wake Zainabu Bakari (19) Mkazi wa Kondoa mkoani Dodoma.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â