December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bashungwa atoa saa Moja kwa mchina kutoa vifaa vya usalama kwa mafundi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amelazimika kutoa viatu vyake vipya na kuwapa Mafundi na kumuagiza Mkandarasi anayeteleza ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma kuhakikisha ndani ya saa moja anatoa viatu vipya na vifaa vya usalama kwa mafundi mafundi wote katika mradi huo.

Bashungwa ametoa agizo hilo wakati akikagua utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Dodoma (Km 112.3) na kutoridhishwa na uchukuaji hatua za usalama kazini kwa wafanyakazi.

Aidha, Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Mohamed Besta, kuhakikisha anasimamia usalama na afya za wafanyakazi mahali pa kazi katika maeneo yote yanapotekelezwa miradi ya ujenzi wa miundombinu kwa kutoa vifaa vya usalama ikiwemo kofia ngumu, viatu, gloves, reflector na barakoa za kuzuia vumbi.