Na mwandishi wetu, TimesMajira online
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI Ndg. Ramadhani Kailima kuwafuatilia watumishi 12 Mkoani Tanga waliogushi barua za Uhamisho na haraka sana warudishwe kwenye vituo vyao vya Kazi.
Mhe. Bashungwa ameongeza kuwa watumishi hao 12 wachukuliwe hatua stahiki za kinidhamu kwa suala la kugushi nyaraka za Serikali.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo
wakati wa Kikao na Waandishi wa habari kuhusu Matokeo ya Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.
More Stories
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
HGWT yawarejesha kwao wasichana 88 waliokimbia ukeketaji
Sherehe Miaka 61 ya Mapinduzi Zanzibar zafana