January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bashe:Uzalishaji mbegu za kisasa kufikia asilimia 70 ifikapo 2025

Na David Johntimesmajira online

SERIKALI inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha inazindua Mashamba 17 yaliowekewa miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji maji  ili yatumike  Katika uzalishaji wa  mbegu za kisasa.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo septemba 8 ,2023 katika kilele cha mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya chakula Afrika (AGRF) na Waziri wa  Kilimo Hussein Bashe ,ambapo Amesema mashamba 17 yanakwenda kutumika katika kilimo cha umwagiliaji .

Bashe akizungumza na waandishi wa habari amesema  Mashamba hayo yatakabidhiwa kwenye Sekta binafsi ya  Watanzania ili wafanye shughuli za uzalishaji wa mbegu za kisasa ambapo Azma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ifikapo mwaka 2025 Nchi izalishe mbegu za kisasa zaidi ya asilimia 70

“Lengo ni kuona mashamba haya 17 yanakwenda katika sekta binafsi na kwa kweli hili ni jambo la rais wetu Dkt Samia ambapo anataka ifikapo 2025 asiliamia 70 ya mbegu za kisasa zizalushwe.”Amesema Bashe

Pamoja na hayo Waziri Bashe ameishukuru Sekta binafsi Kwa uzalishaji wa mbegu hizo Nchini ambapo Watanzania wamezalisha  tani elfu 60  sawa na asilimia 50 ya  uzalishaji wa  mbege hizo.

Wakati huo huo Kampuni ya John dear ya hapa nchini  imeikabidhi Serikali Trekta moja ili iwasaidie vijana  Katika shughuli mbalimbali za Kilimo Nchini na pia Kampuni hiyo Kwa kushirikiana na Serikali itaenda shindano vijna ili kupata kundi la vijana watakaohusika kwenye kilimo Moja Kwa Moja.