November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BASATA yakabidhi vyeti kwa waandaaji wa Miss Tanzania

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) limewapongeza waandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2022 lililofanyika Mei 20 mwaka huu kwa kuwapatia vyeti vya kutambua mchango wao kwa kuonesha makubwa zaidi kwenye Shindano hilo wakiwemo The Look, Quantum Infinity na Startimes Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa makabidhiano hayo hapo leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Matiko Mniko alisema wadau wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki shindano la mwaka huu basi katika mashindano yajayo wandelee kuiunga mkono serikali kuhakikisha sanaa inakua;

“Lengo ni kukutana na wadau wetu walioshiriki waliofanikisha shindano la Miss Tanzania 2022 kwaajili ya kutambua mchango wao na kuwapa pongezi lakini pia kuwapa moyo kuwataka waendelee wao pamoja na wadau wengine ambao hawakupata fursa ya mwaka huu basi hata katika mashindano yajayo na matamasha mengine waendelee kuiunga mkono serikali kuhakikisha kwamba sanaa ya urembo inakua”

Mniko amesema Kwa mwaka uliopita sanaa imekuwa na mchango mkubwa na kukua kwa kasi ya asilimia 19.4 kuliko sekta zote, hii ni fursa pekee kupitia vipaji vya warembo na vijana waliopo ambao wanakua kuanzia ngazi ya vitongoji, Wilaya, Mikoa na Taifa kwa ujumla hivyo wadau wajitokeze kuwashika mikono vijana hao wanaokusudia kuonesha vipaji vyao kwasababu kwa kufanya hivyo itasaidia kujenga uchumi wa nchi yetu

Aidha Mniko alisema Kupitia urembo wamekuwa na watu wengi maarufu ambao wanatumika katika njia mbalimbali za kuleta maendeleo Taifa kwenye Utalii, matangazo ya kibiashara, ubunifu, mitindo n.k;

“Hii kwetu sisi ni fursa ambayo tunapenda kuwaonesha wadau wetu na wawekezaji kwamba katika maeneo mengine tunafikiria kuwekeza basi tuone fursa ya urembo kama ni sehemu kubwa sana ya kuweza kushirikiana na serikali katika maendeleo ya Taifa”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania 2022, Azama Mashango alisesma Serikali imewaunga sana mkono, wamekuwa wakiwasimamia kuangalia wanaenda kwenye mistari ambayo iko sahihi, hivyo wao kama The Loock wanaamini mchango wao unazidi kuwapa nguvu ya kuendelea kwenye shindano lingine la Miss Tanzania.

Aidha wao kama The Look amesema wanaahidi kuendelea kufanya mazuri na kuyaona lakini pia watu wategemee mazuri zaidi kutoka kwao kwasababu wanaamini kama serikali imeweza kutuunga mkono na kuwapongeza basi wanaamini kile wanachokifanya wanakiona.

Naye Meneja Masoko wa Startimes Tanzania, David Malisa alisema wao kama startimes wakihakikisha katika Shindano la Miss Tanzania 2022 linakua la utofauti na pekee, waliweza kuchukua maoni mbalimbali ya watu na kuweza kuyafanyia kazi;

“Utofauti wa shindano hili na mashindano mengine yaliyopita umepatikana kuanzia kwenye content, kuona matukio mbalimbali ya warembo hao wakiwa kambini kupitia kwenye channel yetu ya ST Bongo lakini pia watanzania kutaka shindano lisilo na longolongo kuanzia mshindi na zawadi ambapo vyote hivyo tumevifanyia kazi ambapo kabla hatujaungana na wenzetu The Look tuliweza kwanza kuchukua maoni ya watu nini ambapo wanapenda kiwepo kwenye shindano la Miss Tanzania 2022”

Aidha Malisa aliwataka warembo wote ambao hawakuweza kupata taji la Miss Tanzania 2022 kutokata tamaa na kuendelea kushiriki zaidi katika mashindano yajayo ili kuzidisha kujiamini na kuweza kufanya vizuri