Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Balaza la Sanaa la Taifa BASATA limetangaza vipengele rasmi vitakavyokwenda kushindaniwa na Wasanii wa tasnia ya Muziki katika tuzo za muziki za mwaka 2021.
Tuzo hizi zinalenga kutambua Kazi za Muziki na Wanamuziki waliofanya vizuri kwa mwaka husika kwa kuwapa Tuzo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mtendaji, Matiko Mniko kutoka BASATA amesema vipengele vitakua 23 na ndani ya vipengele hivyo kuna tuzo zipatazo 51
“Vipengele hivyo ni Muziki wa Hip-hop, Muziki wa Bongo Fleva, Muziki wa Dansi/Rhumba/Zouk, Muziki wa Taarab , Muziki wa Reggae /Dance Hall , Muziki wa Singeli , Muziki wa Asili”
Mbali na hayo Mniko amesema Kuna tuzo za mwaka za Wanamuziki binafsi, vikundi na nyimbo shirikishi, tuzo za kazi Bora za Wanamuziki za mwaka, mwanamuziki chaguo la watu jukwaa la kidigitali, tuzo za muziki kimataifa na tuzo za heshima”
Aidha Mniko amezitaja sifa za kuwania tuzo hizo ambazo ni awe ni Raia wa Tanzania na Iwapo Sio Raia wa Tanzania Anapaswa Kuwa na Uthibitisho wa Nyaraka Zitakazomruhusu Kushiriki Zikiwemo Kibali Maalum cha Ukazi na Kufanya Kazi, Awe Amesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa , Kazi Itakayo Wasilishwa na Mshiriki Lazima iwe imesajiliwa COSOTA, Kazi Zitakazowasilishwa Katika Tuzo za Muziki kwa Mwaka 2021 ni Zile Zilizotolewa Kuanzia Tarehe 01/01/2021 Hadi 31/12/2021 na Wanamuziki Wanaofanya Kazi Chini ya Kampuni ni Vyema Kuzingatia Vipengele vya Mikataba Baina Yao na Kampuni Stahiki Wakati wa Kushiriki Katika Tuzo.
Mniko ametoa wito kwa Wasanii na Wadau wa Sanaa wote kupita kwenye mitandao yao ya kijamii yaani Instagram kwa jina la basata.tanzania na Facebook kwa jina la Baraza la Sanaa la Taifa kupata taarifa mbalimbali zinazohusu utekelezaji wa Tuzo za Muziki Tanzania kwa mwaka 2021.
Zoezi la ukusanyaji wa kazi litafanyika kwa siku kumi na nne (14) kuanzia leo tarehe 09 Februari, 2022 hadi tarehe 22 Februari 2022 saa sita (6) usiku. Kazi zitakazokusanywa ndizo zitakazoshiriki katika kuwania Tuzo za Muziki Tanzania kwa mwaka 2021 na si vinginevyo.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba