January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baraza la wazee Kata ya Kilimani laahidi kampeni nyumba kwa nyumba

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

BARAZA la Wazee kata ya kilimani wilayani Dodoma limeahidi kuhakikisha linafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha linakiletea ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo katika mitaa yake minne ya kata ya Kilimani Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa Novemba,14,2024 na Wazee wa Baraza hilo katika kikao chao  kilichokutana katika ukumbi wa Balozi Job Lusindi uliopo katika kata ya kilimani kwa lengo moja la kuhakikisha wanatafuta ushindi wa CCM kwa kishindo kwa viongozi wao walioteuliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama cha Mapinduzi kwa nafasi za wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao wa mitaa yote minne ifikapo Novemba 27 mwaka huu.

Sisi kama Wazee tunamchango mkubwa ya kuelimisha familia zetu na majirani zetu kuwa CCM ndiyo chama bora ambacho kinapaswa kushinda ili kushika Dola kwa kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani 2025.

“Tunajua mchakato mzima wa kuwatafuta wagombea wetu ulifanyika kupitia vikao mbalimbali na sasa waliochaguliwa ndiyo washindi hivyo kwa umoja wetu lazima sasa tuhakikishe tunawanadi vizuri kwa nguvu zote kwa wananchi wa mitaa yote minne na ifikapo Novemba 27,Tujitokeze kwa wingi tukawapigie kura ili kuhakikisha CCM inashinda”walisema kwa kauli moja baraza la Wazee hao

Pia wamekemea vikali suala la makundi yanayao endelea kuwepo sasa baada ya mchakato wa uteuzi kuisha lazima makundi yaishe.

“Sisi kama Wazee tunajua kila Uchaguzi lazima kuwa na kundi lako la ushindi ila baada ya mchakato wa uteuzi wa wagombea basi huwa ni utaratibu wetu katika chama chetu cha Mapinduzi CCM kuhakikisha tunayavunja makundi yote na kubaki na kundi moja tu la wana CCM ili kuweza kukiletea chama chetu ushindi wa kishindo.

“Na tutafanikisha tunapiga kampeni katika kata yetu yote yenye mitaa minne kilimani, Nyerere, Chinyoyo na Image na kampeni yetu itakuwa ya nyumba kwa nyumba kitanda kwa kitanda ili kuhakikisha tunawahamashisha wana CCM na wananchi na wakereketwa wa CCM kuwa ifikapo Novemba 27 kujitokeza kwa wingi kwenye kushiriki kuchagua viongozi wote wa mitaa yote minne wanaotokana CCM.

Kikao kazi hichi ni mwendelezo wa maagizo ya kamati ya siasa kata ya kilimani Jijini Dodoma kilichomwelekeza katibu kata CCM wa kata ya Kilimani kukutana na makundi mbalimbali ya chama hichi ili kwa pamoja kuhakikisha wanakiletea chama cha Mapinduzi kata ya kilimani ushindi wa kishindo.

Makundi mbalimbali atakayo kutana nayo katibu kata CCM kata ya kilimani ni Baraza la Wazee, Jumuiya ya wazazi kata, umoja wa wanawake UWT kata, umoja wa vijana UVCCM kata, kundi la watu wenyewe ulemavu na kundi la maafisa usafirishaji bodaboda kata ya kilimani ikiwa lengo ni kutafuta ushindi wa kishindo wa chama cha Mapinduzi CCM kwa viongozi wao wa mitaa yote minne ifikapo November 27 mwaka huu.

Kwa upande wao wenyeviti wa mitaa yote minne na wajumbe wanao peperusha bendera ya CCM katika kuwania nafasi hizo Novemba 27 mwaka wamesema kuwa Wazee ni hazina kubwa kwa chama cha Mapinduzi hivyo busara zao ni muhimu sana na watahakikisha wakishinda kwenye Uchaguzi watashirikiana nao sana kwa ukaribu katika kuleta maendeleo na kutatua Changamoto mbalimbali zinazo wakabili katika mitaa yao yote minne ya kata ya kilimani ili kuhakikisha CCM na serikali wanashirikiana kwa ukaribu kufanikisha kuzitatua Changamoto mbalimbali zilizopo kwenye mitaa yao.