December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baraza la Madiwani Ilala lapaza sauti ubovu wa barabara

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam limekuja juu kufuatia Ubovu wa Barabara za wilaya kumepelekea Madiwani wa Baraza hilo kupendekeza mapato ya Halmashauri yaelekezwe katika Barabara.

Mapendekezo ya kuekekeza mapato ya Halmashauri yaliozidi kwa mwaka wa fedha 2024 /2025 yalitolewa katika kikao cha Madiwani ukumbi wa mikutano Arnatoglou wilayani Ilala leo na Diwani wa Kata ya Upanga MASHARIKI Sultan Salim.

Diwani Sultan alisema mapato yaliozidi yaelekezwe katika Barabara Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Peke yao hawawezi hata kutafuta Greda za kukodi hivyo Halmashauri lazima tuwasaidie katika hili.

“CHAMA chetu sasa hivi kipo katika mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu 2024 lazima Barabara zipitike katika wilaya yetu Barabara nyingi mbovu tunaishauri Serikali mapato haya yaliozidi yaelekezwe katika miundombinu ya Barabara “alisema Sultan

Diwani wa Kata ya Kisutu Khery Kessy alipongeza Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo pamoja na Mkurugenzi wa jiji Jamary Mrisho Satura na uongozi wa wa Ilala kwa ukusanyaji mapato mwaka huu mpaka kuvuka lengo la Serikali.

Diwani wa Kata ya Pugu Imelda Samjela alishukuru Serikali kwa kumuwekea Lami mita 500 Barabara ya Pugu Majohe ambapo wananchi wa eneo wanajivunia matunda ya Serikali yao.

Diwani wa Kata ya Zingiziwa Wilayani Ilala Maige Maganga, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza mirad mikubwa mbali mbali ya maendeleo kata ya Zingiziwa ikiwemo sekta ya afya,sekta ya Elimu msingi Elimu Sekondari,Masoko na Baadhi ya Barabara.

Diwani Maige Maganga pia alielezea kero ya vivuko na Barabara ameiomba Halmashauri kutatua kero hiyo kata ya Zingiziwa wananchi wa kata hiyo wanapata shida amemuomba Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura Meya wa Halmashauri hiyo Omary Kumbilamoto kusikiliza kilio cha Zingiziwa za Barabara na vivuko