Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam ,Ally Bananga, amesema mabadiliko ya Uongozi katika Baraza la Mawaziri katika Serikali ni sehemu ya Utendaji kazi kawaida ambapo aliwataka waliopewa madaraka Serikali na Chama kuyatumia vizuri katika utekelezaji wa Ilani.
Mwenezi CCM Ally Bananga alisema hayo kata ya Kinyerezi Wilayani Ilala Jimbo la segerea katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi Leah Mgitu.
“Mabadiliko ya uongozi mawaziri ni sehemu ya kawaida umevaa koti sio lako hivyo jiandae kuvua katika uongozi ,kiongozi unatakiwa uwe na heshima ndio maana unaaminika na kupewa madaraka “alisema Bananga.
Ally Bananga ,alisema Chama cha Mapinduzi CCM akitavumilia kwa viongozi wazembe ambao wanatumia madaraka yao vibaya katika utendaji kazi ambapo aliwataka viongozi waliopewa dhamana ya madaraka kufanya kazi kwa weledi.
“Katika mkoa wa Dar es salaam Watendaji wa Serikali wasiotekeleza Ilani achie madaraka mwenyewe akae pembeni awezi kwenda na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutekeleza Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuhudumia wananchi “alisema.
Wakati huo huo katika hatua nyingine ametoa agizo kwa kuwataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa Wilayani Ilala kufanya mikutano ya adhara kuelezea Mapato na matumizi na Mapato waliopokea na kutumia katika mtaa wao.
Alisema Wenyeviti wa Serikali za mitaa wapo katika hatua ya mwisho ya uongozi wao hivyo waeleze utekelezaji wa Ilani vizuri ya chama na wakati wa Daftari la mpiga kura likifika wamasishe wananchi ili waweze kujisajili katika Daftari hilo ili waweze kupata haki ya kupiga kura.
Katika hatua nyingine aliwataka wananchi wa Kinyerezi kulipa tozo ya Takataka usafi sio kupaka wanja bali kulipa tozo ya usafi na Kufanya usafi na kufuata taratibu na kanuni za afya.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini