December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bananga awafunda UVCCM Kinondoni

Na Agnes Alcardo,TimesmajiraOnline,Dar

KATIBU wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amewataka vijana wa CCM Wilaya ya Kinondoni kuwa na umoja ili kukipa chama hicho ushindi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Bananga ameyasema hayo, Agosti 22  alipokua anazungumza na wajumbe wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Kinondoni.

“Vijana mnapaswa kudumisha umoja miongoni mwenu na hiyo ndiyo nguzo ya chama chetu, hususani katika kipindi hiki kuelekeza katika Uchaguzi wa  Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka huu 2024 takwa la kikatiba la CCM ni kushinda uchaguzi na kuongoza Dola”

“Ninyi ndio askari wa Chama hiki, mnapaswa kujua nafasi zenu katika kukihakikishia chama ushindi wa kutosha, lakini pia ninyi wenyewe msiwe wabeba watu tu, Wakati ukifika na ukajipima  nenda kavute fomu ugombee nafasi hizo ni za kwenu pia” amesema Bananga.