December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bambo apewa ubalozi wa Van Beverage

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

KAMPUNI ya Crown royal powerfu ya Dar es salaam imezindua vinywaji maalumu vyenye lengo la kuwachangamsha na kuwaburudisha watanzania kukabiliana na mazingira yaliyopo.

Sambamba na hilo uzinduzi huo umekwenda sambamba na kumtambulisha msanii wa vichekesho nchini Dickson Samson BAMBO kuwa balozi wa kuvitangaza vinywaji vya van beverage ambavyo bei ni nafuu.

Akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam balozi huyo amesema bidhaa hizo ni za kipekee kwa watumiaji lakini humpa ladha ya utofauti mtumiaji yeyote anayevitumia.

“Vinywaji hivi ni Bora na vya kipekee,ladha yake ni nzuri ambayo humuwezesha mtumiaji kujisikia mchangamfu mara tu anapovitumia,” amesema BAMBO

Aidha BAMBO ameeleza kuwa bidhaa hizo ni rafiki kwa watanzania katika kukabiliana na mazingira ya joto au baridi ambapo kauli mbiu ni dogo wa kishua , vinywaji hivyo ni pamoja na van wine, van tangawizi, van whisky pamoja na van vodka.

Kwa upande wake Tx Dullah amesema kuwa bidhaa hizo ni murua na ujazo wa kipee kwa watumiaji ambao hutumia kwa kuongeza na kubadili muonekano wa ndani na nje ya mwili.