January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bakari atoa Ajira kwa vijana wa kusambaza ORYX GAS

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MFANYABIASHARA wa kusambaza Gas ya ORYX Bakari Ahmedy aliyekuwa Diwani wa Bonyokwa atoa Ajira kwa vijana wa Bonyokwa na Wilaya ya Ilala kwa kuwataka watangaze Bidhaa mbalimbali za KAMPUNI ya ORYX GAS kupitia simu za mkononi za Wasap.

Bakari Ahmedy alisema amebuni njia hiyo kutangaza bidha za Gas aina ya ORYX kwa vijana Ili waweze kupata kipato cha chao cha kila siku.

“Makao ,makuu ya Ofisi yetu yapo Bonyokwa standi ya Daladala Jimbo la SEGEREA njia hii ambayo nimebuni kwa vijana watumie simu zao za kiganjani itawawezesha kukua kiuchumi katika kutumia mitandao ya kijamii vizuri na kujenga Mtandao wa Biashara wa ORYX GAS katika kuwamashisha Jamii kutumia Bidhaa za ORYX kuacha kutumia mkaa “alisema Bakari

Bakari alisema vijana walikuwa tayari Katika ajira hiyo ya kutangaza bidhaa za ges ya ORYX mawasiliano yake 0717 78 9992 Ili waweze kujiunga kutangaza bidhaa hizo.

Alisema simu yako ni chombo chako cha muhimu ya kuingizia kipato hivyo kitumike vizuri kwa vijana katika kipindi hichi cha Sayansi na Teknolojia .

“Mimi kama kijana mwenzenu nimeingia mkataba na makampuni ya bidhaa kuchukua mzigo wowote uhusianao mambo ya oryx Gas Tanzania.kama unauwezo wa kumshawishi Mteja na akakubali kununua Bidhaa hizo wewe ni kunipa connection tu kuanzia mteja wa 10000 hadi milioni 100.

Alisema nitampelekea kwa gharama zangu na wewe utalipwa kutokana na ulivyoelewana nae tufanye kazi vijana umri wa mafanikio ndio huo na njia ya mafanikio ni kujituma usisubiri ajira

Alisema unachotakiwa nakupa picha za Bidhaa kazi yako weka status watu wenye mahitaji wakiona wanakupigia na kuulizia bidhaa zako na utauza