January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bajeti ya kilimo yamkuna Mbunge Ditopile, ampongeza Rais samia

Na Penina Malundo, TimesMajira,OnlineĀ 

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini, Mariam Ditopile ameimpongeza Serikali inayoongozwa na Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kutenga bajeti ya kilimo inayokwenda kufanya mapinduzi kwenye sekta hiyo.

Ditopile amesema hayo leo Jumatano  Mei 17, 2022, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo yam waka 2022/23 ya  Bilioni 1751.12  ikiwa imeongezeka kutoka bilioni 294.16.

Akichangia bajeti hiyo, Ditopile amesema, kwa kipindi kirefu bajeti ya kilimo imekuwa ikilalamikiwa na wabunge kwamba ni kidogo lakini mwaka huu imepanda huku akimpongeza Rais Samia kwa kuwateua Bashe kuwa waziri na Anthony Mavumbe kuwa naibu ambao wanaonesha mwanga kwenye sekta hiyo.

“Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kwenye nchi yetu hii ni bajeti ya kwanza inaletwa na Serikali na hakuna mtu analalamika kwamba ni ndogo hapa nimpe pongezi Rais Samia Suluhu Hassan kwa hakika ameonesha yeye ni mkulima mwenzetu na anajali kwa vitendo maslahi ya wakulima nchini na hilo amedhihirisha kwa kutuletea waziri na naibu wake wenye kujali wakulima,” amesema Ditopile

Amesema kilimo kinafanyika sana nchini, ndio maana katika takwimu za Serikali tunaelezwa kilimo kimeajiri asilimia kubwa ya Watanzania, lakini cha kushangaza mkulima anakutana na serikali baada ya kuvuna.

ā€œKilimo ni utafiti na utaalamu, ni udongo ama mbegu, ni sayansi na teknolojia, ni dawa, ni maji kwa maana ya mvua au umwagiliaji, ni miundombinu ya uvunaji, ni urutubisho, ni uhifadhi na ni soko na ukikosoea jambo moja umeondoa tija kwenye kilimo,ā€ amesema Ditopile

Mbunge huyo kutoka Mkoa wa Dodoma amesema wasiache sayansi na teknolojia, waende sawa na dunia.”kwa nini tunakataa mbegu za GMO, tunazikataa kwa nini, tunalima Pamba tunataka kuzalisha nguo, lakini Brazili, India na China wanatumia GMO, sisi tunachokitaka tuleteeni na mkulima aamue, mnasema zina madhara ni uongo mtupu.ā€amehoji

Aidha, Ditopile amezishauri wizara ya kilimo kufanya kazi kwa ukaribu na wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara ili kuwezesha kuwasaidia wakulima kulima mazao yenye tija kwa kipindi fulani.

ā€œNishauri kwamba, tuanzie sokoni, leo hii uhaba wa mafuta ya kula umekuja kujulikana kupitia viwanda vya kibiashara. Niombe wizara ya kilimo na ya biashara mkae pamoja na kushirikiana ili kuwashauri wakulima walime mazao gani yenye tija kwa musimu husikakuwa,ā€ amesema Ditopile na kuongeza:

ā€œBajeti ya kilimo imepanda, niliwahi kushauri vijana lazima watengenezewe namna ya kushiriki kwenye kilimo, naona kundi kubwa hili ambalo nimekuwa mtetezi wao mmewakumbuka na mnakwenda kutoa vitendea kazi na watashiriki sasa kwenye kilimo.ā€amesisitiza

Amesema Bajeti ya kilimo imepanda na imeikumbuka kundi  ya  vijana lazima watengenezewe namna ya kushiriki kwenye kilimo.” naona kundi kubwa hili ambalo nimekuwa mtetezi wao mmewakumbuka na mnakwenda kutoa vitendea kazi na watashiriki sasa kwenye kilimo,”amesisitiza  Ditopile

Bajeti ya Kilimo iliwasilishwa jana Jumanne na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 155.34 ambapo sehemu kubwa ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na miundombinu ya uhifadhi wa mazao.

Pia, kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao, kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu na utoaji wa ruzuku.