Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Bahi
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,Septemba 26, 2024, ametembelea na kukagua baadhi ya vituo vya kujiandikishia kwenye daftari la mpiga kura katika Wilaya ya Bahi ili kuona mwitikio wa wananchi katika zoezi hilo.
Senyamule amejionea namna zoezi hilo linavyokwenda na kupewa taarifa kuwa hakuna changamoto iliyojitokeza tangu kuanza kwa zoezi hilo,Aidha ametumia nafasi hiyo kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.
“Nendeni mkajiandikishe ili mwaka kesho kila mtu mwenye sifa aweze kwenda kupiga kura. Mungu ametupa baraka, Nchi yetu ina demokrasia, kila mtu anatakiwa kupata haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, wajibu wetu ni kuitumia haki hiyo ili kupata viongozi tunaowataka,”Senyamule.
Zoezi hilo lililoanza Septemba 25, linatarajiwa kutamatika Oktoba Mosi, 2024 ambapo Uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura utamuwezesha mwananchi mwenye sifa kupata haki yake ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa Serikali utakaofanyika 2025. Kata zilizotembelewa ni Ibihwa, Mpamantwa na Bahi Sokoni ambapo zote zinaonesha mwitikio mzuri.
More Stories
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini