October 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba, Paroko wahusishwa kifo Cha Asimwe

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”