December 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba kizimbani kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanaye

Na Jumbe Ismailly,TimesMajira Online,Igunga

MKAZI wa Kijiji cha Igunila,Kata ya Ziba,wilayani Igunga,Mkoani Tabora,Sharif Idd Maganga (28) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Igunga akikabiliwa na tuhuma za kumbaka binti mwenye umri wa miaka 14 na kisha kumsababishia ujauzito.

Mapema Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba alidai kuwa kijana huyo ambaye pia ni baba wa kambo wa binti huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130 (1) (2) (e) na 131 (1) kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya 2019 inayozuia kutenda makosa kama hayo.

Mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Igunga,Eddah Kahindi ilidaiwa kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwezi Januari na Agosti mwaka 2020 kwa muda tofauti katika Kijiji cha Igunila,Kata ya Ziba,mshitakiwa Sharif Idd alikuwa akishiriki tendo la ndoa na binti wa miaka 14 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Igunila na hivyo kumsabishia ujauzito.

Kwa taarifa zaidi soma Gazeti la Majira kesho