Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Azam Tv wamezindua tamthiliya mbili zilizobeba simulizi za kuvutia na kuakisi maisha halisi ya watanzania wa rika zote.
Tamthiliya hizo ni ‘Mtaa wa Kaza moyo’ na ‘Lolita’ ambapo zimehusisha waigizaji wenye vipaji na viwango vya juu.
Akizungumza na waandishi wa Habari, msimamizi mkuu wa Sinema zetu, Sophia Mgaza amesema uzalishaji wa tamthiliya hizo umezingatia mahitaji ya soko kwani umetumia vifaa vya uzalishaji vya kisasa na ubora wa Hali ya juu wenye uwezo wa kutoa kazi katika viwango vya picha zenye ubora na angavu.
“Lengo letu la kufanya mambo yote haya ni kuendeleza dhamira yetu ya kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazanaji wetu”
Aidha Mgaza amesema tamthiliya hizo zinachukua nafasi ya fungu langu itakayofikia tarehe 29 Julai 2023 na Jeraha itakayofikia tamati tarehe 10 Agosti 2023.Mgaza amesema burudani zote hizo zitapatikana kwa kifurushi Cha shilingi 8,000 kwa watumiaji wa kisimbuzi Cha dishi na antena.
Kuhusu Tamthiliya ya Mtaa wa kazamoyo na Lolita, zikesanifiwa kwa uangalifu mkubwa ili kuwapa watazamaji aina mbalimbali za simulizi za hadithi zenye kulinda maadili ya kitanzania, kutoa elimu kwa jamii na zinazotazamika na familia yote.
Aidha Tamthiliya hizo zinajumuisha viwango vya juu vya uzalishaji na mbinu za hali ya juu ili kuhakikisha utazamaji wa kuvutia kwa hadhira
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba