Na Oscar Assenga, TimesMajira Online, Tanga
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa hatashindwa kuendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu ikiwemo kuwapokonya kazi wakandarasi wanaosuasua ikiwemo wanaokwamaisha utekelezaji wa miradi ya maji nchini
Kauli hiyo alilitoa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya maji mkoani Tanga ambapo amesema kuwa katika kutekeleza tayari ameshawafuta kazi jumla ya wakandarasi 118 pamoja na makampuni 69 yaliyokuwa yanaendesha miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha inampatia mwananchi huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yake bila ya kulazimika kutembea umbali mrefu lakini uwepo wa huduma ya uhakika.
“Uhandisi wa maji ni pamoja na kufuatilia miradi uliyopewa n a kujiridhisha kama huduma ipo, pale unapo sema Mradi umekamilika basi inamana unatoa maji kwa asilimia 100% na sio ujanja ujanja”amesema Waziri Aweso.
Amewataka wataalamu wabadili fikra zao juu ya utekelezaji wa miradi ya maji akitolea mfano miradi ya maji vijijini una sehemu tatu ya kwanza ni chanzo eneo la pili tanki la maji la tatu ni kituo cha usambazaji au kama kuna eneo lenye maji ya mserereko lazima kuwea na eneo la kitibu maji.
“Sasa unajenga chanzo, unajenga tenki la maji, unatandaza vituo vya maji halafu unaangiza pump miezi sita watu wanaona vituo vya maji lakini maji hayatoki unatengeneza malalamiko, manung’uniko na masononeko yalisiyo na ulazima “amesema Waziri Aweso.
“Kwa hiyo hizo ndio fikra ambazo lazima zibadilike kwenye wizara ya maji unapojenga intake ya maji agiza pampu ili twende sambamba watu waweze kuyatumia maji kuhakikisha dhamira ya Rais wetu Samia Suluhu inatimilika”amesema
More Stories
Wafanyabiashara wakutana Dar,kujadili hali ya biashara
Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ubelgiji lafanyika Dar
CCM kuhitimisha kampeni kwa kishindo