Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini Nchini, Askofu William Mwamalanga, amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan, kuendelea kufanya marekebisho makubwa taasisi za fedha ili wananchi wa hali chini waweze kuingia kwenye biashara ndogo ndogo na kubwa.
Aidha, Askofu Mwamalanga amesema wananchi wengi wanaachwa mbali kutokana na uwezo mdogo wa kifedha huku wengine wakiingia kwenye mikopo kausha damu.
Askofu Mwamalanga alitoa ushauri huo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Alisema Rais Samia akifanyia taasisi za fedha mabadiliko makubwa zitawezesha wananchi kupata mikopo kwa urahisi na kuondokana na mikopo ya kausha damu.
Aidha, alimshauri Rais Samia kuingilia kati ili Wazabuni wanaolisha shule na vyuo waweze kulipwa madeni yao ambayo wanadai kwa muda mrefu. “”Hawa Wazabuni ndiyo wanalisha watoto chakula kwenye vyuoni na shule za bweni lakini wengine hawajalipwa kwa miaka mawili hadi leo..
Serikali inapolipa madeni kwenye taasisi na watu binafsi kama Wazabuni na makandarasi kwa wakati njamii ya chini inanufaika kwani hao ndiyo vibarua.
“Baadhi ya Wazabuni kutoka mikoa ya Rukwa , Katavi na Songwe wameonesha kukataa tamaa kutokana na madhara makubwa yanayo wakutana kwa zaidi ya miaka mitatu ya kukosa fedha za malipo yao. .Alisisitiza kwamba Serikali inapochelewesha malipo ya wazabuni inahatarisha afya wanafunzi vyuoni na mashuleni
More Stories
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari