Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha waliotimiza miaka ishirini na mbili kazini wametoa msaada katika kituo cha faraja Orphanage kilichopo shangalai wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha ikiwa ni mchango wao kwa kituo hicho cha kulea watoto yatima na wahitaji.
Akiongea kwa niaba ya askari wenzake Sajenti MWANEMA amesema wameona ni vyema kutoa msaada huo ambao umenda sambamba na shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwalinda kipindi cha miaka ishirini na mbili kazini.
Aidha amebainisha kuwa imekuwa ni utamadunia wa askari Polisi kutoa msaada kwa makundi yenye uhitaji ambapo amewaomba watu wengine kutoa walicho nacho kwa watoto wenye uhitaji katika vituo vya watoto yatima.
Nae Mkurungenzi wa faraja orphanage Mchungaji Faraja Malaki amewashukuru askari hao kwa mchango na msaada wao katika kituo hicho na kuwaomba wengine wenye moyo wa kujitoa wafike kituo cha faraja kusaidia watoto hao wenye uhitaji.
Nae Jephason Faraja ambae ameongea kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika kituo hicho amewashukuru askari hao kwa kutoa msaada huo ambao umefanya wajisikie ni kundi linalokumbukwa katika Jamii.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba