January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Askari wakike watakiwa watakiwa kushiriki operesheni za kulinda amani

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kamishna wa Jeshi la Polisi Tanzania Suzan Kaganda amewahamasisha washiriki wa mkutano wanne wa mafunzo wa Jumuiya ya Polisi wa kike duniani (IAWP) Ukanda wa Afrika kutumia elimu wanayoendelea kupata ili kufahamu maana ya ulinzi wa amani na kushiriki katika opereshini mbalimbali za kimataifa.

Ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo amewaeleza askari hao kufahamu kwa kina kuwa wanapokwenda kulinda raia wengi katika mataifa yenye changamto ya amani waathirika wa kubwa katika operesheni hiyo wao ni wanawake na Watoto ambapo amebainisha kuwa wanatakiwa kuwa na ufahamu wa mambo mengi yatakayo wasaidia katika kulinda amani.

Kamishna Kaganda ameongeza kuwa askari hao wanatakiwa kuongeza sifa za ziada kitaluma ambazo huangaliwa na Umoja wa Mataifa, Pia amemshukuru Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kiongozi wa mafano kwa askari wa kike kwa kukubali Mkutano huo kufanyika Nchini Tanzania.

Kwa upande wake Karani wa Mahakama kutoka Nchini Ghana Bi Selasi Tachie Selasi mbali na kupongeza mafunzo hayo amesema ipo sheria ya 2007 Nchini Ghana inayoongoza namna ya kushugulikia maswala ya ukatili wa kijinsia ambapo amebainisha kwa kuja kwake Tanzania amejifunza mengi ya namna ya shughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia.

Pia Mkaguzi msadizi wa Jeshi la Magereza Beatha Benard Nyasegwa amesema wamejifunza namna ya urekebisha wa Jamii hususani inayoletwa Magerezani namna ya kuwarekebisha.

wanapokuwa magerezani na wanapotoka magerezani Kwenda uraiani ambapo amewaomba wananchi kuwapokea pindi wanapomaliza vifungo vyao.