January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Asasi za Kiraia zaaswa kuhimiza matumizi sahihi ya teknolojia

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Asasi za kiraia zimeaswa kuhakikisha kuwa zinaendelea kuhamasisha jamii matumizi bora ya teknolojia ili teknolojia hizo ziwe msaada kwa jamii

Hayo yameelezwa jijini Arusha leo na mkurugenzi mtendaji wa Foundation for civil society Bw Francis Kiwanga Wakati akiongea kwenye ufunguzi wa mkutano wa wiki ya asasi za kiraia

Francis amesema kuwa asasi za kiraia zina mchango mkubwa sana hasa kwenye sekta ya teknolojia ambapo wana uwezo wa kuisaida jamii kujua na kutambua aina ya teknolojia ambayo itaweza kuwasaida kwenye maendeleo

“kuna teknokojia ambazo zinaweza kusaidia jamii hizo ambazo zinaweza kusaidia jamii sasa zinatakiwa zipewe kipaumbele ili ziweze kuleta tija kwenye jamii”ameongeza

katika hatua nyingine ameitaka jamii kuhakikisha kuwa wanaenda sambamba na mabadiliki ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kutumia teknolijia ambazo zitaongeza ufanisi zaidi.

Naye mwakilishi wa kampuni ya Apple ambaye pia naye ameongea katika mkutano, Abubakary Ally alisema kuwa jamii ya kitanzania inapaswa kuhakikisha inakubaliana na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kusimama na teknolojia moja ambayo itazaaa matunda

Abubakary amesema kuwa teknolojia ina nafasi kubwa katika kuleta maendeleo endapo tu mtumiaji atahakikisha kuwa anatumia vyema ikiwa ni pamoja na kupata ujuzi wa teknolijia hiyo ipasavyo.

Awali akiongea kwa niaba ya Meya wa jiji la Arusha,diwani wa kata ya ngarenaro Isaya Doita amesema kuwa kwa sasa teknolojia imekuwa kwa kiwango kikubwa sana lakini bado jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia teknolojia ipasavyo na sio kwenda kinyume na teknolojia hizo.

Doita amesema kuwa ili teknolojia ziweze kutumika ipasavyo hata kwa jamii ni muhimu kwa waaandishi wa habari lakini pia vyombo vya habari kuhakikisha kuwa vinaeleza umuhimu wa teknolojia na matumizi yake ambayo ni mazuri ili teknolojia hizo ziweze kuleta mabadiliko ndani ya jamii.