Na Penina Malundo,timesmajira
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewashukuru Watumishi wa afya wote walijitokeza kuhudumia majeruhi katika ajali ya ndege iliyotokea katika Mkoa wa Kagera iliyotokea Novemba 6, 2022.
Dkt. Mollel ametoa pongezi hizo leo alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ambapo kwa jitihada za Watumishi wa afya mpaka kufikia leo alibaki majeruhi mmoja tu.
Aidha, Dkt. Mollel amesisitiza Serikali itaendelea kugharamia majeruhi wote waliotokea katika ajali hiyo ya ndege mpaka watakapokuwa sawa kiafya.
Sambamba na hilo, Dkt. Mollel amempongeza Rais wa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya za Watanzania kwa kuendelea kuboresha miundombinu kama majengo ya dharura na kuwapa mafunzo Wataalamu ambao kwa kiasi kikubwa wamesaidia katika kuokoa hali ya majeruhi waliokuwa katika ajali ya ndege.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba