January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Arusha yaweka mikakati kusaidia shule zinazoongoza mithiani ya Taifa

mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa uongozi wote wa mkoa wa Arusha umeweka mikakati ya kusaidia shule zote ambazo zinafanya vizuri na kuongoza kwenye mithiani ya kitaifa ikiwa ni pamoja na kuwapa vipaumbele mbalimbali

mbali na kuwapa vipaumbele hasa kwenye masuala ya elimu pia bado mkoa unataka kuona shule nyingi zikiingia kwenye ushindi wa shule bora kitaifa kama ambavyo shule ya wavulana Tengeru boys inavyofanya kwa sasa。

Hayo yameelezwa na John Mongela jumamosi iliopita kwenye maafali ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya wavulana Tengeru Boys ambao wanatarajia kufanya mthiani wao hivi karibuni.

Mongela alisema kuwa shule ambazo zinafanya vizuri katika mithiani ya kitaifa ni muhimu sana kusaidiwa na mkoa wa Arusha ili zisikwame kwa lolote lile bali ziendeleee kutangaza jina la mkoa

“tumeshaweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa pale juu kwenye shule bora na sisi tupo hapo na ndio maana hata leo napenda sana niwapongeze Tengeru Boys kwa kuwa kila mthiani wa mwisho wa kitaifa huwa mnatuheshimisha Arusha”alisema

Wakati huo huo aliwataka wazazi ambao wanatabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani kuacha na badala yake wawatoe ili waweze kupata haki yao ya msingi ya elimu

“leo hapa pia kuna waitimu ambao ni walemavu wa kusikia ni furaha sana kuwaona wapo vizuri na ninaambiwa wanafanya vizuri sana kwenye mithian je wangefungiwa ndani tuamke jamani hawa watoto wanatakiwa kupata elimu tena sahihi”aliongeza

Naye Mkurugenzi wa shule hiyo ya Tengeru Boys Father John Assey kutoka shirika la roho mtakatifu aliitaka jamii kuachana na tabia ya kutowapa kipaumbele watoto viziwi badala yake wahakikishe wanapata elimu sawa na wengine.

“ninasema hivyo kwa kuwa nina ushaidi kwenye mthiani uliopita tuna kijana mmoja ambaye ni kiziwi ambaye alifanya vizuri sana na kupata daraja la kwanza kabisa wakati huo huo kwenye mashule mengine kuna waliopata sifuri na wanasikia tusukubali jamani hawa watoto wakakaa bila elimu”aliongeza Father Assey

Alifafanua kuwa ili kuendelea kuboresha mazingira ya vijana ambao ni.viziwi shuleni hapo wanatarajia kuanza utaratibu wa kuwapima kiwango cha usikivu ambapo kwa kufanya hivyo kutaruhusu kuwafanya wanafunzi hao kusoma bila ya kupata changamoto yoyote ile.

Naye mkuu wa shule hiyo.Bw Gaudence Mtui alisema kuwa wanafunzi hao ambao wanatarajia kuanza mithiani yao hivi karibuni wameandaliwa vyema kimasomo lakini hata kimaadili

Mtui aliwataka wazazi wa wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanakuwa mstari wa mbele hasa kuwalinda na maadili mabaya kwa kuwa ndani ya shule wamepikwa kwenye maadili mazuri