December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

APC Hotel kinara wakutoa fursa kwa Vijana

WAKATI Maonyesho ya 48 ya Kimataifa ya Kibishashara yakiendelea kushika kasi katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Kituo cha Mikutano APC Hotel and Conference Centre kimepongezwa kwa kuendelea kutoa Elimu jinsi ambavyo kituo hicho kimeendelea kutoa huduma kwa Jamii pamoja na kuzalisha ajira mbalimbali kwa vijana Nchini.

Hayo yamebainishwa leo Julai 06,2024 na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA. Prof. Sylvia S.Temu wakati alipo tembelea banda la Kituo hicho katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere

Amesema Kituo hicho cha APC kimekuwa kikitoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za hoteli, kumbi za mikutano zenye uwezo wa kubeba watu wengi.

Aidha CPA Prof. Sylvia Temu amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikitoa Fursa za ajira kwa vijana na kuwataka watanzania kuendelea kuchangiamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi

Katika hatua nyingine CPA Prof. Sylvia Temu ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kutembelea banda hilo ilikujionea jinsi ambavyo Kituo hicho kimekuwa kikiendelea kuvutia wawekezaji kupitia huduma mbalimbali.