Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya mawasiliano ya Yas imezindua rasmi kampeni yake mpya ya ‘Anzia Ulipo’ katika hafla fupi iliyofanyika jijini Mwanza.
Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha Watanzania kutumia teknolojia kama chombo cha kuanzisha na kuendeleza ndoto zao mahali walipo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Masoko wa Yas, Edwardina Mgendi amesema kampeni ya Anzia Ulipo ni mwito mahsusi kwa kila Mtanzania kuona fursa zilizopo katika dunia ya kidijitali na kuchukua hatua sasa.

Hata hivyo amesisitiza kuwa, mafanikio hayahitaji ukamilifu bali uthubutu wa kuanza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa ameeleza kuwa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla zina nguvu kubwa ya kiuchumi kupitia uvuvi, kilimo, biashara na ubunifu, hivyo ni eneo muafaka kwa kampeni hiyo.
Kampeni hiyo imekuja wakati ambao matumizi ya teknolojia yanakua kwa kasi katika kanda hiyo, huku takwimu za TCRA zikionesha kuwa Kanda ya Ziwa ni ya pili kwa matumizi ya data na huduma za kidijitali nchini.

Hiyo inaashiria utayari wa wakazi wake kushiriki kikamilifu katika mapinduzi ya kidijitali.
Yas, imewekeza katika upanuzi wa miundombinu ya mawasiliano, ikiwemo mtandao wa 4G na 5G, ili kuwasaidia Watanzania.
Lengo ni kusaidia vijana, walimu, wakulima na wajasiriamali kutumia teknolojia kwa mafanikio ya kweli katika shughuli zao za kila siku.


More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10