Na Esther Macha , Timesmajira Online, Mbeya
MWANAUME mmoja ambaye hajafahamika makazi yake mkoani Mbeya amewauwawa kwa kuchomwa moto na wananchi wa kata ya Isanga wenye hasira kali baada kudaiwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka (5) mpaka kufa .
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ,Shadrack Isaya amesema kuwa alikuwa ametoka kwenye shughuli zake akiwa anarudi nyumbani akasikia harufu ya kinyesi kwenye pagala.
“Kwangu ni lazima ukatishe kwenye hili pagala ndo nifike nyumbani kwangu katika kusogea nikasikia harufu ya kinyesi kwenye hilo pagala wakati juzi tu tumetoka kufanya usafi kutokana na watu kumwaga taka, Sasa baadae niliyosikia harufu tena ya kinyesi nikahisi labda kuna mlevi anajisaidia nikawasha taa ilikuwa Kama saa 1.45 usiku nikamuona jamaa kalala chini huku suruali akiwa ameishusha chini “amesema shuhuda huyo.
Akielezea zaidi shuhuda huyo amesema kwamba alipowasha taa ya simu akazima na kuwasha mtu huyo akainuka na kuanza kuvaa suruali yake na kugundua chini kuna mtoto mdogo wa kiume kalala chini nikapanda kwenye gema akampiga teke na mtuhumiwa huyo akampiga jiwe shuhuda baadaye mbakaji akaanza kumshambulia kwa maneno shuhuda huku akiwa ameshika kisu na kumwambia shuhuda utakufa kishamba .
“Nilianza kupiga kelele na watu walijitokeza na kuanza kumpiga mbakaji huyo huku Mimi na watu wengine tukimbeba yule mtoto na kwenda nae hospitali , nilivyokwepa kisu kilikuwa kinakuja kichwani nilikikwepa na kupiga kofia “amesema.
Shuhuda mwingine ,Hadija Bintimasudi ambaye ni Balozi wa mtaa huo amesema alikuwa ametoka mnadani kujumua nguo alipoingia ndani akiwa na wajukuu zake ndani kwake akiwa anapanga nguo wakasikia sauti nje za kelele za kumlawiti mtoto na kukuta mtoto hana nguo.
Amesema kuwa wananchi wenye hasira hatujui kilichotokea mpaka mtu kuwawa na matukio hayo yamekuwa yakitokea mara nyingi ya kupotea watoto na kupatikana wakiwa hai lakini hili la safari hii limetisha.
Baba mzazi wa mtoto huyo , Benjamin Mwashilindi amesema kwamba alikuwa safarini akitokea Makambako kikazi alipigiwa Simu akiwa mlima nyoka na kuambiwa mtoto wake kabakwa ilibidi achukue bodaboda ili awahi nyumbani na alipofika eneo la tukio alikuta mtuhumiwa hayupo kauwawa na kufanikiwa kuona mabegi tu na kuchukua jukumu la kumpigia Mwenyekiti kuuliza hospitali waliyoenda na kuwakuta hospitali ya rufaa ya mkoa.
Mwenyekiti wa mtaa Igoma A Kata ya Isanga, Damian Mwasanguti amesema kuwa mtuhumiwa huyo si mkazi wa maeneo hayo na kusema kwamba wakiwa hospitali walipata taarifa kuwa mtuhumiwa ameuwawa kwa kuchomwa Moto na mwili wake kuchukuliwa na polisi.
Amesema kuwa Kwa tukio kama la jana likiwa la kwanza kutokea ingawa watoto walikuwa wanapotea lakini walikuwa wanapatikana.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato