December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Amrabat amaliza matembezi Hifadhi ya Taifa Mikumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kiungo wa Timu ya Manchester United ya Uingereza, Sofyan Amrabat ambaye pia huchezea kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa ya Moroko, amemaliza kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Morogoro ambapo kwa maneno yake akionesha kufurahia safari yake amepost akitania: “Tanzania, East Africa: Leo Simba wa Atlas (jina la utani la nchi yake) Amekutana na Simba Mwenyewe!” Awali Amrabat alikuwa ametembelea visiwa vya Karafuu Zanzibar!

Mastaa kadhaa wanatembelea kufanya shughuli za utalii duniani wakati huu wa mapumziko ambapo Tanzania inazidi kuwa moja ya maeneo pendwa.

Beki wa mabingwa wa soka wa Ufaransa PSG, Ashraf Hakimi naye yupo nchini kwa mapumziko.