December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ameir:Hakuna Mwekezaji atajayejutia kuwekeza Zanzibar

Na Penina Malundo, timesmajira

NAIBU Waziri wa Mipango na Fedha Ally Suleimain Ameir amesema hakuna mwekezaji atakayekuja kujutia kuwekeza katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu ina fursa nyingi za kiuchumi.

Akizungumza jana katika siku maalumu ya Zanzibar iliyofanyika viwanja vya maonesho ya 47 ya kitaifa (sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam,alisema kwa kuhakikisha kuwa Zanzibar ina fursa mbalimbali hadi sasa kuna ongezeko la asilimia 39 ya watalii nchini wanaotembelea mji huo.

“Mwaka 2021 kulikuwa na jumla ya watalii 394.185 na mwaka 2022 kulikuwa na watalii 548503 na kusababisha kuwa na ongezeko la asilimia 39″amesema Naibu Waziri Ameir.

Aidha amesema kwa mwaka 2022 katika Serikali hiyo tayari jumla ya miradi 97 iliwekezwa yenye takribani ya thamani ya sh.bilioni 4.5.

“Tumejipanga kuwakaribisha wawekezaji na ndio maana hivi sasa tunawawezesha wafanyabiashara wetu ili wafanye vizuri na tumerudisha siasa ya ustaarabu ili kudumisha amani na ulivu siku zote”amesema

Akizungumzia maonesho ya Sabasaba, Naibu Waziri huyo amesema maonesho hayo yanafungua ushirikiano mzuri kati ya nchi na nchi na kuzidi kuongeza ushirikiano baina ya watu.

“Maonesho haya yanafungua fursa za biashara kwa wafanyabiashara na kutangaza biashara ndani na nje ya nchi”amesema

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) Latifa Hamisi Abdallah amesema lengo la kuwa na siku maalumu ya Zanzibar ni kuangalia kipaumbele gani walichonacho kwa lengo la kuwatangazia watanzania.

“Mimi najua Zanzibar kuna fursa nyingi na nzuri hapa leo tutaonyesha fursa chache tu “amesema