January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ama’z Auction Mart yazamilia kufanya makubwa sekta ya Udalali

Na Heri Shaaban

KAMPUNI ya Udalali AMA’Z Auction Mart imejipanga kufanya mambo makubwa katika sekta ya udalali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa AMA’Z Auction Mart Dawa Jumanne wakati wa kuzungumza na Waandishi wa habari kuelezea mikakati ya kampuni hiyo na mafanikio yake.

Dawa alisema Kampuni ya AMA’Z Auction Mart imeanzishwa Julai Mwaka huu imesajiliwa inatoa huduma zake hapa nchini

Dawa alisema Kampuni ya AMA’Z inajishughulisha kukusanya kodi na ushuru, kudai madeni, kuuza vitu mbalimbali kama vile nyumba, viwanja, samani, kufanya minada, kupangisha, kuratibu safari za kitalii, kukusanya taka hatarishi na kutao ushauri wa kiufundi.

Alisema Mikakati ya kampuni hiyo wanatarajia kufungua matawi katika kila kanda hapa nchini pamoja na kujitanua nje hasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Tunashukuru katika kipindi cha muda mfupi tangu tuanzishe kampuni yetu tumepokelewa vizuri kwani baadhi ya taasisi za Serikali, taasisi binafsi na watu mbalimbali wametupa ushirikiano mkubwa,” alisema Dawa.

Amewashauri wateja kutafuta madalali ambao wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria ili yanapojitokeza matatizo yanayohusiana na shughuli za udalali wawe na haki ya kisheria.

Aidha alisema wanawakaribisha wenye kampuni, taasisi na wananchi mbalimbali walioko ndani na nje ya nchi wanaotaka kuuza au kununua vitu mbalimbali waitumie kampuni yetu ya AMA’Z

Alisema wanapopata kazi za kudai madeni huwa hawatumii nguvu kubwa bali hushauriana na mdaiwa husika na kama ikishindikana ndivyo wanachukua hatua zingine.

“Hatutumii nguvu kubwa kudai madeni tunatafuta suluhu kwa kuzungumza na mdaiwa husika na pale tunapoona imeshindikana ndiyo nachukua hatua zingine tunawashauri watu wanaodaiwa kama na taasisi za fedha wakiwa na matatizo wasikae kimya wawe wazi na kuzieleza taasisi husika kwa sababu ukikaa kimya riba inazidi kuongezeka,” alisema.

Pia alisema hadi sasa kampuni hiyo imetoa ajira kwa zaidi ya vijana 200 kuunga mkono juhudi Rais wa ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda kuwakwamua kiuchumi wananchi.