November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Amana vijana center kitovu cha maarifa

Wahitimu wa chuo cha Amana vijana centre jijini Dar es Salaam wakiwa na nyuso za furaha baada ya kuhitimu mafunzo ya kozi zao.

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

CHUO cha Amana vijana centre Dar es salaam, kimetajwa kuwa kitovu cha maarifa kwa vijana kuweza kujiajiri ama kuajiliwa.

Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Meya na diwani wa makongo Joseph Rwegasira amesema chuo cha Amana ni kitovu cha maarifa kwa vijana wetu kujipatia ujuzi.

Hayo yamejiri jijini katika mahafali ya 24 yaliyofanyika katika ukumbi wa panand i panandi uliopo katika kata ya Ilala ambapo jumla ya vijana 129 walihitimu wakiwemo wavulana 42 na wasichana 87.

“Serikali ya awamu ya sita imejipambanua kuendeleza sekta ya elimu nchini hivyo chuo hiki ni kitovu cha maarifa kwa vijana wetu,”amesema Rwegasira

Rwegasira amesema ni fursa kwa wazazi,ndugu kuwapeleka vijana wao kwa lengo la kujipatia mafunzo yatolewayo na chuo hicho.

Aidha naibu hiyo amedai Serikali ipo pamoja nao katika utatuaji wa changamoto mbalimbali ikiwemo mikopo kwa vikundi ambapo kiongozi huyo ameahidi kutoa viti.

Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo hicho Philipo Ndokeji amewataka wahitimu kuzingatia taaluma kuwa ni nyenzo bora pamoja na nidhamu huko waendako .

Hata hivyo mkuu huyo ameeleza miongoni mwa kozi wazitoazo ni pamoja na hoteli Management,upambaji, saluni,kompyuter,ufundi wa magari na kiingereza.

Nae mhitimu wa kozi ya hoteli Bilali Ally amedai kuitendea haki taaluma aliyoipata na kushauri vijana wengine kujiunga na chuo hicho.