December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ali Kiba awajibu wanaosema ananunua Watazamaji Youtube

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva na Bosi wa King Music, Ali Kiba amewajibu wale wote wanaosema kuwa yeye ananunua watazamaji katika mtandao wa Youtube jambo ambalo si la kweli.

Akiwapa majibu hayo, baada Ya Minong’ono hiyo Kuwa mingi Ali Kiba amemjibu moja kati ya Tweet ya Shabiki ambaye aliandika kuwa msanii huyo ananunua views.

”Siwezi kujitekenya na kucheka mwenyewe,” amejibu Ali Kiba.

Hata hivyo, msanii huyo yupo mbioni kuachia ngoma mpya hivi karibuni baada ya kupost Video Katika Ukurasa wake wa Twitter akiwa anaimba wimbo huo wenye maneno;

”Walitaka niwe chini, ukanipandisha, mapenzi yako siwezi kufananisha, bora nikushukuru.’kuwa tayari wimbo huu unakuja muda si mrefu”.