Na Allan Vicent, TimesMajira Online
KUKAMILIKA kwa mradi wa maji ya chemchem uliotekelezwa na RUWASA katika vijiji vya Kichacha na Chilambo kata ya Kasanda Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma kumeleta neema kubwa kwa akinamama na wakazi wote wa vijiji hivyo.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti akinamama wa kata hiyo wamemshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi yake ya kuwatua ndoo kichwani.
Joyce Jacob (40) mkazi wa Kitongoji cha Kichacha amesema akinamama wa kata hiyo sasa hivi hawahangaiki tena kwenda mabondeni kutafuta maji.
‘Tuliteseka sana kwa kutembea umbali mrefu na ndoo kichwani, kwa kweli mama yetu Samia ametuokoa’, amesema.
Naye Mekisiana Mikael (39) mkazi wa Kijiji cha Chilambo ameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao cha maji na kuwapelekea mradi huo.
‘Akinamama na wakazi wote wa kata hii tunamshukuru sana mama kwa kupata mradi huu na tunachangia hela kidogo tu kila kila ndoo ni sh 20,’ amebainisha.
Meneja wa RUWASA Wilayani hapa Mhandisi Brighton Benjamin ameeleza kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha sh mil 891 na wakazi wote wa kata hiyo zaidi ya 3500 sasa wanapata maji safi na salama kwa masaa 24.
Ameongeza kuwa kata zote zina maji safi ila baadgi miradi inaendelea kutekelezwa ikiwemo kata ya Kasuga ambayo ilikuwa na changamoto kubwa sana.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza