Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Watumishi 91 waliopata ajira mpya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na waliohamia 11 wametakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika Hospitali hapo.
Akizungumza leo katika ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Julieth Magandi amewataka watumishi kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi ambao hufika hospitalini hapo kwa mahitaji mbalimbali.
Dkt. Magandi ameeleza kuwa kulingana na idadi kubwa ya wananchi wanaohudumiwa na Hospitali hiyo huduma bora ndio kitu pekee kinachoweza kuifanya Hospitali hiyo kuendelea kuheshimika.
“Tuna wateja wa ndani na wateja wa nje, huduma bora ndio kitu cha msingi kwetu” amesisitiza Dkt. Magandi.
“Tunataka kila mtu atakayekuja hapa apate huduma bora, ili hata akienda huko atangaze kuwa amehudumiwa kwa viwango stahiki.” amesisitiza Dkt. Magandi.
Ameongeza kuwa Hospitali hiyo inahudumia wananchi zaidi ya 4,000 kwa siku ambao kila mmoja anahitaji huduma bora.
More Stories
Shaka:Uimara wa Rais Samia ni matokeo chanya unaojali kesho ya nchi
Dkt.Batilda:Tumeanza mazungumzo waliotelekeza viwanda wanyang’anywe
TMA:Kuna ongezeko la joto kwa baadhi ya maeneo nchini