Na Penina Malundo, timesmajira
AJALI za majini ni miongoni mwa janga kubwa kwa mataifa mbalimbali
Ajali hizi zimekuwa zikizikumba nchi nyingi duniani ambapo takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)zinaonyesha ya kwamba vifo vinavyoyotokana na watu kuzama katika maji ni asilimia saba ya vifo vyote vinavyotokana na ajali mbalimbali duniani kote.
Karibu watu takribani 236,000 duniani hupoteza Maisha kutokana na kuzama katika maji kila mwaka,
inaonyesha kwamba ni ndogo ukilinganisha na uhalisia wake.
Udogo huo wa takwimu na udhaifu na mapungu katika ukusanyaji wa takwimu na taarifa za ajali duniani kote .
Imelezwa kuwa matukio ya ajali majini yanaripotiwa kuwa chini ya asilimia 50 ya matukio yote huku asilimia 90 ya vifo vya kwenye maji vinatokea katika nchi zinazoendelea ,zenye kipato cha Chini na cha kati.
Akizungumza hivi karibuni, Mkurugenzi
wa idara ya utafiti Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI),Dkt. Mary Kishe kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Uvuvi kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi ,Emmanuel Bulayi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ajali za kuzama majini na athari zake,anasema umoja wa mataifa umeamua kulizungumzia suala hili la
kuzama majini kwa ustawi wa idadi kubwa ya watu duniani kote.
Anasema mnamo April 2021 jumuiya ya kimataifa upitia umoja wa mataifa ilijadili na kuridhia kwamba siku ya julai 25 ya kila mwaka iwe siku rasmi ya kukumbusha nchi zote duniani kuchukua hatua.
Anasema ni vema nchi zote duniani kuchukua hatua stahiki ili kuweza kuzuia vifo vitokanavyo na kuzama
majini katika maeneo ya pwani,baharini kwenye maziwa na mito ili kokoa kwa kiasi kikubwa Maisha ya watu.
“Katika kusherehekea siku hiyo umoja wa mataifa pamoja na mambo mengine unasisitiza nchi wanachama kuchukua hatua stahiki kulingana na
mazingira ya kitaifa kama kuweka kituo kikuu cha kitaifa cha kuzuia kuzama maji na kutengeneza mpango wa Taifa wa kuzuia kuzama maji,”anasema na
kuongeza
“Pia kutengeneza program za kuzuia kuzama maji zinazokwenda sambamba na uingiliaji uliopendekezwa na shirika la Afya Duniani,kuhakikisha kukuza mwamkowa umma juu ya kulinda na kuzama maji na kufanya kampeni ya badilitabia na kufikiria uanzishwaji wa mafunzo ya msaada wa dharura ,usalama majini na uogeleaji
Aidha anasema kupitia maadhimisho haya ni vema kujenga uelewa wa pamoja juu ya athari zitokanazo na
ajali za kuzama kwenye maji na jinsi ya kuchukua tahadhari.
“kuhakikisha kuwa umma wa watanzania wanapata taarifa juu ya vifo vitokanavyo na kuzama kwenye
maji ili kuweza kushirikiana na wadau mbalimbali kuokoa Maisha ya maelfu ya wavuvi,mabaharia na wasafiri wanaotumia njia ya maji,”anasema
Anasema Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA),tayari wameanza kutoa mafunzo ya usalama (safety at
sea) kwa wanaoendesha na kutumia
vyombo vidogo vidogo.
“Mafunzo hayo ambayo yana ithibati ya TASAC yanatolwqa katika kampasi za FETA zilizoko Bagamoyo ,Mwanza,Kigoma na Mtwara ambapo mpaka sasa jumla ya wananchi 2,600 wamepatiwa mafunzo hayo yanayolenga kupunguza ajali na vifo vya kwenye maji visivyo vya lazima.
Anasema nchi yetu imekwisha kuridhia mikataba ya kimataifa inayohusu viwango vya ubora katika utoaji wa mafunzo kwa wavuvi na mabaharia.
“Serikali inaamini kwamba utoaji mafunzo kwa wavuvi na mabaharia kwa kuzingatia vigezo hivyo utatusaidia sana kupunguza tatizo la ajali za kwenye maji pia serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha maadhimisho hayo yanaendana na makubaliano ya umoja wa mataifa ili kupunguza au
kutokomeza kabisa vifo vitokanavyo na kuzama maji kwa jamii za wavuvi na wadau wengine,”anasema
Naye Ofisa Uvuvi Emedo ,Grace Kakama anasema suala la usalama wa wavuvi wanapokuwa kazini ni muhimu sana kwani wanakumbana na changamoto nyingi wanapokuwa baharini.
Anasema miongoni mwa Changamoto wanazokumbana nazo ni Pamoja na vyombo wanavyotumia kuwa duni hali inayosababisha wanapokuwa wanafanya shughuli ya uvuvi
wanaweza kukutana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupelekea kuwepo katika hatari ya kuzama wakati mwingine kupoteza maisha.
“Unakuta usiku huo mvuvi anapozama,nertwork ya simu imekata kutokana na eneo waliopo kutokuwa
na mawasiliano na kushindwa kuwasiliana na watu waliopo nyumbani hivyo kuwafanya kukosa msaada
wakati huo,”anasema na kuongeza”Tunashukuru jumuiya ya kimataifa, imeona kwamba kuna umuhimuMkubwa sana wa kuhakikisha tunalinda maisha ya uvuvi kwakuweka rasmi siku ya kimataifa ya kujenga uelewa juu ya ajaliza majini na jinsi ya kuepuka hivyo manispaa ya Kinondoni inafurahakubwa katika hili kwani tumekuwa tukipokea taarifa mbalimbali za vifo vya wavuvi kwa wastani tumekuwa tukipokea taarifa ya vifo vya watu wa nne hadi watano kwa mwezi wanaofariki kutokana na ajali za majini inatokana mitubwi imezama au upepo kuwa mkali,”anasema kakama.
Anasema vifo vya wavuvi vinavyotokea mara nyingi vinakuja kusikika pindi ndugu wa karibuwasipomuona mpendwa wao au pale mwili unapookotwa pembezoni mwa bahari.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO),Editrudith
Lukanga,anasema kupitia maadhimisho hayo wameweza kuufahamisha umma wa watanzania
juu ya umuhimu wa kupata taarifa juu ya vifo vitokanavyo na kuzama kwenye maji ili kuweza kushirikiana na wadau mbalimbali kuokoa maisha ya maelfu ya wavuvi, mabaharia, na wasafiri wanaotumia njia ya maji.
***Akizungumzia kuhusu Zanzibar
katika maadhimisho hayo
Meneja wa mradi wa kujenga uhimilivu wa wakulima wa mwani Zanzibar kutoka Milele Zanzibar
Foundation,Ali Rashid Hamad anasema katika kufikia azma hiyo ya kuzuia watu kuzama taasisi yao imefanikiwa kutoa mafunzo ya kuogelea kwa wakulima wa zao la mwani.
Anasema tayari wakulima 300 wa zao hilo la mwani wamepatiwa mafunzo hayo kutoka Unguja na Pemba ili
waweze kulima zao hilo kwenye kina
kirefu cha maji na si kulima tena kwenye kina kifupi cha maji.”Tumeona kuna hatari kubwa ya wakulima hao kuweza kuzama hivyo kutokana na suala hilo tumeamua kuwafundisha kuogelea wakulima hao ambao wengi hao ni wamama ili waweze kulima kwenye kina kirefu kwani zao hili linastawili vyema
katika kina kirefu cha maji na kwa sasa tumeanza kuona mabadiliko wanalima kwenye kina
kirefu,”anasema.
Meneja wa Taasisi ya Panje anasema ili kuhakikisha kuna punguzo la vifo vitokanavyo na kuzama kwa maji kama maazimio yaliotolewa na Umoja wa
mataifa ya kuzuia kuzama taasisi hiyo imeanza kutoa mafunzo ya kuwagusa walimu 88 kuogelea kwa
shule za Unguja na Pemba ili kuwafundisha wanafunzi.
Anasema baada ya walimu hao kupata mafunzo hayo walimu hao wataweza kuwafundisha vijana ambao ni
wanafunzi kwenye shule zao jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya vifo vitokana navyo na kuzama na
maji.
More Stories
Ubunifu wa Rais Samia kupitia Royal Tour unavyozindi kunufaisha Tanzania
Rais Samia anavyojenga taasisi imara za haki jinai kukabilina na rushwa nchini
Rais Dk. Samia alivyowezesha Tanzania kuwa kinara usambazaji umeme Afrika