December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ajali za barabarani zatajwa kuwa chanzo cha ugonjwa wa kifafa

Na Mwandishi wetu Timesmajira online

KATIKA Kuelekea siku ya Kifafa duniani ambayo uadhimishwa siku ya Jumatatu ya pili ya mwezi Februari Chama cha Kifafa Tanzania(T.E.A) kimesema ajali za barabarani ikiwemo za bodaboda zimekuwa kisababishi kikubwa cha ugonjwa wa kifafa nchini.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam jana Daktari bingwa wa Mishipa,Fahamu,Ubongo na Uti wa mgongo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH),Patience Njenje wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema maadhimisho ya mwaka huu yatafanyika Februari 14 yakiwa yamebebwa na kauli mbiu ya” Kifaa ni zaidi ya degedege”

Amesema pindi mgonjwa anapopata ajali hasa katika maeneo ya kichwani upelekea kuwepo kwa kovu katika ubongo na badae kupelekea kupata ugonjwa wa kifafa.

“Kati ya wagonjwa tunaowapokea hapa hospitali wengi wao waliopata ajali mbalimbali hasa bodaboda na kukikuta wanaumwa ugonjwa wankifafa kutokana na ubongo kupata itilafu ikiwemo makovu ambapo wengi wao ni
vijana wenye umri wa miaka 15 “alisema

Dkt Njenje alibainisha kuwa mtu anapopata ajali kichwani humsababishia kovu kwenye ubongo na kusababisha kupata ugonjwa wa Kifafa.

Amesema kisababishi kingine ni pamoja na kuanguka chini kwa watu wazima na watoto mara kwa mara kusababisha makovu katika ubongo, ambayo husabisha degedege za mara kwa mara nakuwa kifafa.

Sababu nyingine ya kupata kifafa usababishwa na degedege la utotoni ambalo uleta kovu katika ubongo, mtoto asiyetoka kwa wakati wakati wa kujifungua anakosa hewa na kusababisha ubongo wake kupata makovu, vivimbe katika ubongo, minyoo hasa ya nguruwe

Vilevile amesema kuwa minyoo aina Tape Worm inayopatikana katika nyama ya Nguruwe ambayo haijaandaliwa vizuri nayo uweza kusababisha Kifafa hivyo mtu anapokula minyoo hiyo upitia katika damu na kwenda katika ubongo na kusababisha ugonjwa wa kifafa.

Dk Njenje akizungumzia hali ya ugonjwa huo nchini alisema kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa kifafa wapatao zaidi ya milioni moja , hivyo inaongoza kati ya mataifa ya Afrika na dunia wagonjwa wengi ni vijana wa miaka 15.

Dkt Njenje amesema katika vijiji vya Mahenge Morogoro na Idom Manyara inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wa kifafa ambapo kati ya watu 1000 wa eneo hilo 37 wanaugua ugonjwa huo,

Alisema.kwa upande wa eneo la Idom mkoani Manyara minyoo inayopatikana ni Tape Worm ambayo imekuwa ikisababisha ugonjwa huo.

Dkt Njenje amesema Kwa upande wa eneo la Mahenge minyoo wanapopata wakazi wa eneo aina ya Onchocerciasis inatokana na wadudu aina ya Mbung’o anapong’ata minyoo hiyo hupitia kwenye damu na kwenda kwenye ubongo.

Alizitaja takwimu za dunia za watu wenye kifafa alisema zaidi ya watu milioni 60 wanaishi na kifafa, alisema ongezeko la watu 34 hadi 76 kwa kila watu 200,000 kwa mwaka.

Amesema watu wenye ugonjwa wa kifafa wapo kwenye hatari ya kifo mara sita zaidi ya watu wasio na ugonjwa huo. Pia alisema zaidi ya asilimia 60 ya vifo vinasababishwa na athari za ugonjwa wa kifafa moja kwa moja au kwa namna nyingine.

Amesema maadhimisho ya ugonjwa wa kifafa uadhimishwa kila wiki ya pili ya mwezi Februari ambapo mwaka huu yataadhimishwa Februari 14, siku ya wapenda nao, ambapo kauli mbiu itakuwa ni ‘Kifafa ni zaidi ya degedege’.

Dkt Njenje amesema kifafa ni ni kitendo cha kupata degedege zaidi ya mara mbili kwa siku. Pia alifafanua kuwa Degedege utokea pale ubongo unapopata kovu za majeraha mbalimbali ambayo uzuia umeme kutembea na kusambaa katika ubongo.

Aidha ameitaka jamii kuachana na imani potofu ikiwemo ushirikina, kwakuwa ni moja ya njia ya kuongezeka kwa ugonjwa huo katika jamii.

Pichani ni daktari Bingwa wa mishipa, Fahamu ubongo na utii wa mgongo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) Patience Njenje akizungumza na waandishi wa habari