Na Rose Itono,Timesmajira
Airtel Tanzania imekabidhi hundi ya Sh. bilioni 73.9 kwa serikali na kuibuka mshindi wa pili kwa mashirika yaliyotoa gawio kubwa kwa mwaka 2024/25
Akizungumza mara baada ya hafla ya siku ya Gawio iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Ikulu Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Eliudi Sanga, amesema kujituma kwa Airtel kuna mchango mkubwa katika kuchochea mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Amesema Airtel Tanzania inajivunia kuwa mshirika wa kuaminika katika safari ya maendeleo ya taifa, Uwekezaji wake unaendana na vipaumbele vya kitaifa kwa kupanua miundombinu ya kidijitali na kuchangia upatikanaji jumuishi na wezeshi wa uchumi wa kidijitali
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Charles Kamoto, amesema malengo ya Airtel ni
kuwezesha ukuaji jumuishi na uwezeshwaji wa kidijitali.
“Mchango wa gawio letu ni kielelezo cha msimamo wetu katika kuchagiza kwenye maendeleo endelevu ya Tanzania. Hii inaakisi namna sera ya serikali inavyoendana na ubunifu wa sekta binafsi katika kuleta maendeleo jumuishi na kuelekea katika uchumi wa kidigitali,” amesema Kamoto.
Amesema Airtel
inajivunia kuiunga mkono serikali kupitia uwekezaji wake kupitia upanuzi wa mtandao, unafuu wa vifaa vya mawasiliano na majukwaa ya kidijitali nchini Tanzania.
Hata hivyo kwenye hafla hiyo Rais Dkt Samia
ametoa shukrani kwa mashirika na Taasisi binafsi kwa kuchangia sh. Tirion 1.28 kwa mwaka huu
Dkt Samia amesisitiza kuwa serikaliI inaendelea kuweka mazingira bora ili kuendelea kuchochea uwekezaji na kuongeza kasi ya ukuaji kiuchumi
More Stories
Kiongozi wa Mwenge aifagilia RUWASA Tanga
Rais Samia kuanza ziara ya siku saba Simiyu na Mwanza
Msigwa awataka wazazi kuzungumza na watoto wao matumizi mabaya ya mtandao