Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MSEMAJI wa timu ya soka ya Klabu ya Simba Ahmed Ally amesema ni wakati muafaka sasa kwa wadau wa soka kujiunga na mfumo wa Kielektroniki wa ununuzi wa umma (NeST) unaotumika na Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA) ili nao waweze kupata tenda za serikali kupitia mfumo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi ya PPRA jijinini Dodoma,Ahmed amesema mfumo huo ni umerahisisha uombaji wa zabuni za Serikali lakini pia umeweka wigo mpana kwa wananchi kushiriki katika zabuni hizo.
Ametumia nafasi hiyo kuipongeza PPRA kwa kujenga mfumo huo ambao unaondoa matabaka katika upatikanaji wa zabuni hizo ambao awali olikiwa mpaka ujuane na mtu ndipo upate tenda.
Amesema akiwa kama mdau wa soko amelibeba jambo hilo ambapo kwa kushiriliana na Ally Kamwe wanakwenda kulizungumza suala hilo kwa mapana yake ili watu wengi hasa wafanyabiashara kujiunga na kutumia mfumo huo.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Denis Simba amesema, kuna fursa kubwa kwenye michezo kupitia tenda za Serikali ambazo zipo kwenye Mfumo wa NeST.
Amesema Matokeo ya sasa kwenye tasnia ya michezo ni ushindi hulu akisema matokeo hayo yasiishie kwenye ushindi nafuraha tu bali yaende mbalimbali hasa katika fursa za kiuchumi lupitia mfumo wa NeST.
Aidha Simba amesema , takribani asilimia 70 ya bajeti ya Tanzania ni ununuzi kupitia mfumo wa NeST ambayo ni zaidi ya sh.Trillion 20 na kupitia mfumo kuna fursa nyingi za wanamichezo katika tenda za Serikali.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria