December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Afisa Mtendaji Liwiti ahamasisha Sensa

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

AFISA MTENDAJI wa kata ya Liwiti Iginas Maembe Leo amezindua kampeni ya sensa katika miaka mitatu ya Umoja wa michezo new Lada jogging iliyopo Liwiti Wilayani Ilala.

Katika uzinduzi huo ulienda sambamba na hamasa ya michezo kutoka TABATA mpaka Liwiti na jumbe mbalimbali za sensa .

Akizungumza mara baada kuitimisha maandamo hayo ya miaka mitatu ya Lada jogging alisema dhumuni la siku hiyo ni kuisaidia Serikali katika kutoa elimu kuisaidia zoezi la Kitaifa la Serikali Sensa ya makazi AGOSTI 2022 kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.

“umoja wa jogging Lada ni kikundi cha hamasa pamoja kijamii kinashirikiana na Serikali katika kazi mbalimbali matukio ya Serikali leo tumeanza kampeni ya kutoa elimu kwa ajili zoezi la sensa ya makazi” alisema Maembe.

Afisa Mtendaji Maembe aliwashukuru wadau mbalimbali ambao wamefanikisha sherehe hiyo akiwemo DIWANI wa kata ya Liwiti , Katibu wa CCM Liwiti na Katibu wa Umoja wa Wanawake Mtaa wa Amani Geni Malaki.

Alitoa wito kwa Wananchi wa Liwiti watoe ushirikiano Katika zoezi la anuani za makazi ambalo linaendelea kila kata nchini.

Mwenyekiti wa Lada jogging Liwiti Poul Mtambo dhumuni la michezo hiyo kujenga umoja na mshikamano sambamba na kuwaweka vijana wakue katika maadili mema .