Na Herishaban, TimesMajira Online, Ilala
Afisa Mazingira halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Rajabu Ngoda, ameongoza kampeni ya Usafi wilayani Ilala leo ambapo Kikanda kampeni hiyo imefanyika soko la Kigogo Sambusa .
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Afisa Mazingira halmashauri hiyo Rajabu Ngoda, alisema kampeni hiyo ni endelevu ambapo ni utaratibu unafanyika kila mwezi.
” halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo tumeendeleza kampeni ya usafi katika soko la Kigogo sambusa na Barabara ya kawawa tumefanya usafi kwa kushirikiana na Kampuni za usafi” alisema Ngoda .
Afisa Mazingira Ngoda aliwataka wananchi wa Wilaya ya Ilala kujenga tabia ya usafi katika kutunza Mazingira na kusafisha mitalo inayowazunguka katika Mazingira yao biashara zao .
Ngoda aliwataka wananchi na wafanyabishara kujenga tabia ya usafi na kuzibua mitalo katika maeneo yao ya biashara na makazi katika kujiandaa kuelekea mvua za vuli na El Nino ambazo zinatarajia kuanza mwezi Octoba mwaka huu.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu