Na Mwandishi wetu, Timesmajira
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amesema Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe kuwa mipango ya uwezeshaji wa wakulima inapaswa kujikita vijijini ili kuwawezesha wakulima halisi na kuongeza tija katika uzalishaji.
Amesema kuna mradi huu wa BBT. Fikra ya kuwawezesha wakulima ni fikra njema,lakini, mpango ulipaswa kujikita vijijini. H”uko ndiko waliko Wakulima halisi,mtindo wa wizara kukusanya vijana mijini, kuwapa mikopo, ardhi na nyenzo, hautaleta matokeo makubwa na mpango utafeli kama ilivyofeli mipango iliyotangulia ya kilimo”,amesisitiza Ado
“Janga la ajira ni bomu linasubiri kuripuka. Ili kukabiliana nalo, pamoja na mambo mengine ni lazima tuboreshe kilimo na shughuli nyingine za uzalishaji vijijini kwa kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za uhakika, bei nzuri za mazao na mikopo yenye riba nafuu kuongeza tija katika kilimo na ufugaji”-amesema Ado.
Katika hatua nyingine, Ado amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ibane matumizi na kuzuia ubadhirifu ili kuhakikisha kuwa inaajiri zaidi hasa kwenye maeneo ambayo yana mahitaji makubwa ya wafanyakazi kama vile walimu, madaktari na maafisa ugani.”Serikali ya CCM imechoka kifikra. Kila Mwaka CAG anaonesha mabilioni ya Watanzania yanaliwa.
Serikali ingeongeza udhibiti kwenye eneo hilo ingeweza kuokoa fedha nyingi na kuajiri wahitimu wengi zaidi ambao kwa miaka mingi bado wapo mtaani”- amesema Ado
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa