December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ADC yamuomba Rais Samia kuruhusu mikutano ya hadhara

Na Rose Itono,Timesmajira

CHAMA Cha Alliance For Democratic Change (ADC) kimeiomba Serikali ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa Ili viweze kujiimarisha

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa Mkutano wa Bodi ya Uongozi wa Chama hicho Mwenyekiti ADC Hamad Rashid Mohamed alisema kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara kunaathiri sana utendaji wa vyama vya siasa

“ADC tunaamini sana utendaji kazi wa Rais wa awamu ya sita katika utekrlezaji wa masuala mbalimbali yanayohusisha haki hivyo tunaamini na hili la kuviruhudi vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara atalufanyia kazi kwa haraka,” amesema Hamad

Pia ameongeza kuzitaka Taasisi zinazotanya mabadiliko ya kisiasa kuwashirikisha wadau na kuongeza kywa kufanya maamuzi ya mabadiliko yeyote pasipo kuwashirikisha ni kosa kisheria

Aikizungumza hali halisi ya mfumuko wa bei za vyakula kunakoikabili nchi kwa Sasa aliiomba Serikali kuumiza kichwa na kwamba ADC Iko tayari kutoka msaada

Kwa upande wa tatizo la Maji Hamad amesema nchi yetu Ina vyanzo vingi vinavyoweza kuwezesha kupatikana kwa Maji ikiwepo mito

‘ Ilani yetu ya uchaguzu kwa mwaka 2015 tulisema na ingelikywa wanatekeleza sera ya ADC leotusingekuwa na tatizo hilo nchini,’aliingeza Hamad na kuongeza kuwa nchi Ina napato tatizo ni udhibiti wa napato hayo

Ametolea mfano kwa kusema kipindi Cha COVID Shughuli mbalimbali ziliktwa zukifanywa kidigitali badala ya kutumia makaratasi hali ambayo ilipunguza gharana kwa kiasi kikubwa na kubana natumizi

Amesema natumizi ya kidigitaliyatawezesha nchi kupunguza gharanaziluzokywa zinatumika kupitia makaratasi na fedha zitakaxodhibitiwa zitawezesha Shughuli zingine za kimaendeleo

Amesema endapo Chama Cha ADC kitashika Dora kitatumia zaidi natumizi ya kidigitali Ili kuipunguzia Serikali nzugo wa kutumia gharana kubwa kwenye uendeshaji wake wa Shughuli za kiutendaji

Mkutano huu wa Bodi ya Uongozi umewashirikisha wajumbe mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Visiwani.