January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ACT Wazalendo yalia kukua kwa deni la Taifa

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema kuwa kasi ya kukua kwa deni la Taifa ambalo limefikia Tsh. Trilioni 91.7 ukilinganisha na Tsh. Trilioni 77 za Mwaka uliopita, kunaongeza ugumu wa maisha kwa sababu Serikali inatumia mapato yake mengi kuhudumia deni hilo.

Akizungumza na wananchi katika Jimbo la Bariadi Mkoani Simiyu amesema kuwa katika Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, katika kila Tsh. 1000 itayokusanywa na Serikali, Tsh. 370 imepangwa kuhudumia deni la taifa.

“Fedha hizi zingepaswa kutumika kuwaletea maendeleo kwenye afya, barabara na maji, inabidi zitumike kulipa deni. Tunatoa rai kwa Rais Samia, badala ya kuongeza bidii kwenye kukopa, tuongeze bidii kwenye kudhibiti mianya ya rushwa na ubadhirifu,”amesisitiza Ado.